Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ruthu 4:13 - Swahili Revised Union Version

13 Basi Boazi akamtwaa Ruthu, naye akawa mke wake; naye akaingia kwake, na BWANA akamjalia kuchukua mimba, naye akazaa mtoto wa kiume.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Kwa hiyo, Boazi akamchukua Ruthu akawa mke wake. Mwenyezi-Mungu alimjalia Ruthu naye akachukua mimba, akajifungua mtoto wa kiume.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Kwa hiyo, Boazi akamchukua Ruthu akawa mke wake. Mwenyezi-Mungu alimjalia Ruthu naye akachukua mimba, akajifungua mtoto wa kiume.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Kwa hiyo, Boazi akamchukua Ruthu akawa mke wake. Mwenyezi-Mungu alimjalia Ruthu naye akachukua mimba, akajifungua mtoto wa kiume.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Basi Boazi akamtwaa Ruthu, naye akawa mke wake. Alipoingia kwake, Mwenyezi Mungu akamjalia Ruthu, naye akapata mimba, akamzaa mtoto wa kiume.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Basi Boazi akamwoa Ruthu, naye akawa mke wake. Alipoingia kwake, bwana akamjalia Ruthu, naye akapata mimba, akamzaa mtoto wa kiume.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

13 Basi Boazi akamtwaa Ruthu, naye akawa mke wake; naye akaingia kwake, na BWANA akamjalia kuchukua mimba, naye akazaa mtoto wa kiume.

Tazama sura Nakili




Ruthu 4:13
12 Marejeleo ya Msalaba  

Abrahamu akamwomba Mungu, Mungu akamponya Abimeleki, na mkewe, na wajakazi wake, nao wakazaa wana.


Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.


BWANA akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai.


Yakobo akamghadhibikia Raheli, akasema, Je! Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia uzao wa mimba?


Akainua macho yake, akawaona wale wanawake na watoto, akauliza, Ni nani hawa walio pamoja nawe? Akasema, Ni watoto Mungu aliompa mtumwa wako kwa neema yake.


Humweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha.


Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa BWANA, Uzao wa tumbo ni thawabu.


Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana watu wote wa mjini wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema.


Nyumba yako na ifanane na nyumba yake Peresi, ambaye Tamari alimzalia Yuda, kwa wazao atakaokupa BWANA katika mwanamke huyu.


Niliomba nipewe mtoto huyu; BWANA akanipa dua yangu niliyomwomba;


Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Lakini waliokuwa na njaa sasa hawana njaa tena. Naam, huyo aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini aliye na watoto wengi amehuzunika.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo