Obadia 1:18 - Swahili Revised Union Version18 Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa muali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa BWANA amesema hayo. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema18 Wazawa wa Yakobo watakuwa kama moto na wazawa wa Yosefu kama miali ya moto. Watawaangamiza wazawa wa Esau kama vile moto uteketezavyo mabua makavu, asinusurike hata mmoja wao. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND18 Wazawa wa Yakobo watakuwa kama moto na wazawa wa Yosefu kama miali ya moto. Watawaangamiza wazawa wa Esau kama vile moto uteketezavyo mabua makavu, asinusurike hata mmoja wao. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza18 Wazawa wa Yakobo watakuwa kama moto na wazawa wa Yosefu kama miali ya moto. Watawaangamiza wazawa wa Esau kama vile moto uteketezavyo mabua makavu, asinusurike hata mmoja wao. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu18 Nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto; nayo nyumba ya Esau itakuwa bua kavu, nao wataiwasha moto na kuiteketeza. Hakutakuwa na watakaosalimika kutoka nyumba ya Esau.” Mwenyezi Mungu amesema. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu18 Nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto; nayo nyumba ya Esau itakuwa bua kavu, nao wataiwasha moto na kuiteketeza. Hakutakuwa na watakaosalimika kutoka nyumba ya Esau.” bwana amesema. Tazama suraBIBLIA KISWAHILI18 Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa muali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa BWANA amesema hayo. Tazama sura |
Kwa hiyo kama vile muali wa moto uteketezavyo mabua makavu, na kama manyasi makavu yaangukavyo katika muali wa moto; kadhalika shina lao litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi, na kulidharau neno lake aliye Mtakatifu wa Israeli.
Siku hiyo nitawafanya wakuu wa Yuda kuwa kama kigae chenye moto katika kuni, na kama kinga cha moto katika miganda; nao watateketeza watu wa kila kabila, wawazungukao pande zote, upande wa mkono wa kulia na upande wa mkono wa kushoto; na baada ya haya Yerusalemu utakaa mahali pake, naam, hapo Yerusalemu.