Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Nehemia 5:13 - Swahili Revised Union Version

13 Tena nikakung'uta nguo yangu, nikasema, Mungu na amkung'ute vivyo hivyo kila mtu nyumbani mwake, na kazini mwake, asiyeitimiza ahadi hiyo; naam, na akung'utwe vivyo hivyo, na kuwa hana kitu. Mkutano wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA. Nao watu wakafanya kama walivyoahidi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Nilikunguta kibindo changu na kusema, “Kila mmoja asiyetimiza ahadi hii Mungu na amkungute, amtoe katika nyumba yake na katika kazi yake. Basi, akungutike na kubaki mikono mitupu.” Mkutano mzima ukaitikia, na kusema, “Amina” wakamsifu Mwenyezi-Mungu. Watu wakafanya kama walivyokuwa wameahidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Nilikunguta kibindo changu na kusema, “Kila mmoja asiyetimiza ahadi hii Mungu na amkungute, amtoe katika nyumba yake na katika kazi yake. Basi, akungutike na kubaki mikono mitupu.” Mkutano mzima ukaitikia, na kusema, “Amina” wakamsifu Mwenyezi-Mungu. Watu wakafanya kama walivyokuwa wameahidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Nilikung'uta kibindo changu na kusema, “Kila mmoja asiyetimiza ahadi hii Mungu na amkung'ute, amtoe katika nyumba yake na katika kazi yake. Basi, akung'utike na kubaki mikono mitupu.” Mkutano mzima ukaitikia, na kusema, “Amina;” wakamsifu Mwenyezi-Mungu. Watu wakafanya kama walivyokuwa wameahidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Pia nikakung’uta makunjo ya vazi langu na kusema, “Kila mtu ambaye hatatimiza ahadi hii, Mungu na amkung’ute hivi kutoka nyumba yake na katika mali yake. Basi mtu kama huyo akung’utiwe nje na aachwe bila kitu!” Waliposikia hili, mkutano wote ukasema, “Amen,” na wakamtukuza Mwenyezi Mungu. Nao watu wakafanya kama walivyokuwa wameahidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Pia nikakung’uta makunjo ya vazi langu na kusema, “Kila mtu ambaye hatatimiza ahadi hii, Mungu na amkung’ute hivi kutoka nyumba yake na katika mali zake. Basi mtu wa namna hiyo akung’utiwe nje na aachwe bila kitu!” Waliposikia hili, mkutano wote ukasema, “Amen,” na wakamtukuza bwana. Nao watu wakafanya kama walivyokuwa wameahidi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

13 Tena nikakung'uta nguo yangu, nikasema, Mungu na amkung'ute vivyo hivyo kila mtu nyumbani mwake, na kazini mwake, asiyeitimiza ahadi hiyo; naam, na akung'utwe vivyo hivyo, na kuwa hana kitu. Mkutano wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA. Nao watu wakafanya kama walivyoahidi.

Tazama sura Nakili




Nehemia 5:13
17 Marejeleo ya Msalaba  

Mfalme akasimama karibu na nguzo, akafanya agano mbele za BWANA, kumfuata BWANA, na kuyashika maagizo yake, na shuhuda zake, na amri zake, kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kuyathibitisha maneno ya agano hilo yaliyoandikwa katika kitabu hicho; nao watu wote wakalikubali agano lile.


Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, tangu milele hata milele. Na watu wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA.


Ezra akamhimidi BWANA, Mungu Mkuu. Nao watu wote wakaitika, Amina, Amina, pamoja na kuinua mikono yao; kisha wakainamisha vichwa vyao, wakamsujudu BWANA kifudifudi.


Nimeapa nami nikathibitisha, Kuzishika hukumu zako za haki.


Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye Juu nadhiri zako.


Wekeni nadhiri na mziondoe Kwa BWANA, Mungu wenu. Wote wanaomzunguka wamletee hedaya, Yeye astahiliye kuogopwa.


Wao waiachao sheria huwasifu waovu; Bali wao waishikao hushindana nao.


Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe.


na maji yaletayo laana yatakuingia matumboni mwako, na kukuvimbisha tumbo, na kukupoozesha paja lako; na mwanamke ataitika, Amina, Amina.


Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung'uteni mavumbi ya miguuni mwenu.


Nao wakawakung'utia mavumbi ya miguu yao, wakaenda Ikonio.


Walipopingana naye na kumtukana Mungu, akakung'uta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu; mimi ni safi; tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa.


Kwa maana wewe ukibariki kwa roho, yeye aketiye katika mahali pa mjinga ataitikaje, Amina, baada ya kushukuru kwako, akiwa hayajui usemayo?


Basi Samweli akamwambia, Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo