Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 49:27 - Swahili Revised Union Version

27 Benyamini ni mbwamwitu mwenye kuraruararua Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 “Benyamini ni mbwamwitu mkali; asubuhi hula mawindo yake, na jioni hugawa nyara.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 “Benyamini ni mbwamwitu mkali; asubuhi hula mawindo yake, na jioni hugawa nyara.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 “Benyamini ni mbwamwitu mkali; asubuhi hula mawindo yake, na jioni hugawa nyara.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 “Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye njaa kuu; asubuhi hurarua mawindo yake, jioni hugawa nyara.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 “Benyamini ni mbwa mwitu mlafi mwenye njaa kuu; asubuhi hurarua mawindo yake, jioni hugawa nyara.”

Tazama sura Nakili




Mwanzo 49:27
25 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.


Na wana wa Benyamini; Bela, na Bekeri, na Ashbeli, na Gera, na Naamani, na Ehi, na Roshi, na Mupimu, na Hupimu, na Ardi.


Baraka za baba yako Ni nyingi kuliko za milima ya kale, Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake, yeye aliyeteuliwa kati ya ndugu zake.


Hayo yote ndiyo makabila ya Israeli kumi na mawili. Na hayo ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa baraka zake aliwabariki.


Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwamwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi.


Fitina ya manabii wake imo ndani yake, kama simba angurumaye akirarua mawindo; wamekula roho za watu; hutwaa kwa nguvu hazina na vitu vya thamani; wameongeza idadi ya wajane wake ndani yake.


Wakuu wake kati yake wamekuwa kama mbwamwitu wakirarua mawindo; ili kumwaga damu, na kuharibu roho za watu, wapate faida kwa njia isiyo halali.


Wakuu wake walio ndani yake ni simba wangurumao; mahakimu wake ni mbwamwitu wa jioni; wasiobakiza kitu chochote mpaka asubuhi.


Katika wana wa Benyamini, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;


Tazama, watu hawa wanaondoka kama simba jike, Na kama simba anajiinua nafsi yake, Hatalala hadi atakapokula mawindo, Na kunywa damu yao waliouawa.


Katika kabila la Benyamini, ni Elidadi mwana wa Kisloni.


Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.


Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali.


Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwamwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;


Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.


Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu,


Akamnena Benyamini, Mpenzi wa BWANA atakaa salama kwake; Yuamfunika mchana kutwa, Naye hukaa kati ya mabega yake.


Nilitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila la Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,


Wana wa Benyamini wakatoka Gibea, wakawaua watu elfu ishirini na mbili katika Israeli siku hiyo.


Benyamini alitoka kupigana nao kutoka Gibea siku ya pili, wakawaua watu elfu kumi na nane tena katika watu wa Israeli; hao wote walikuwa wamejihami.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo