Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 47:26 - Swahili Revised Union Version

26 Yusufu akaifanya kuwa sheria ya nchi ya Misri hata leo, ya kwamba sehemu ya tano iwe mali ya Farao. Ila nchi ya makuhani tu haikuwa mali ya Farao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Ndivyo Yosefu alivyotangaza sheria moja ambayo iko mpaka leo nchini Misri: Kila raia lazima atoe sehemu moja ya tano ya mavuno yake kwa Farao. Ardhi ya makuhani tu ndiyo haikununuliwa na kufanywa mali ya Farao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Ndivyo Yosefu alivyotangaza sheria moja ambayo iko mpaka leo nchini Misri: Kila raia lazima atoe sehemu moja ya tano ya mavuno yake kwa Farao. Ardhi ya makuhani tu ndiyo haikununuliwa na kufanywa mali ya Farao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Ndivyo Yosefu alivyotangaza sheria moja ambayo iko mpaka leo nchini Misri: kila raia lazima atoe sehemu moja ya tano ya mavuno yake kwa Farao. Ardhi ya makuhani tu ndiyo haikununuliwa na kufanywa mali ya Farao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Basi Yusufu akaiweka iwe sheria ya ardhi katika nchi ya Misri, ambayo inatumika hata leo, kwamba sehemu ya tano ya mazao ni mali ya Farao. Ni ardhi ya makuhani tu ambayo haikuwa ya Farao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Basi Yusufu akaiweka iwe sheria kuhusu nchi ya Misri, ambayo inatumika mpaka leo, kwamba, sehemu ya tano ya mazao ni mali ya Farao. Ni nchi ya makuhani tu ambayo haikuwa ya Farao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

26 Yusufu akaifanya kuwa sheria ya nchi ya Misri hata leo, ya kwamba sehemu ya tano iwe mali ya Farao. Ila nchi ya makuhani tu haikuwa mali ya Farao.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 47:26
11 Marejeleo ya Msalaba  

Ahimidiwe Mungu Aliye Juu Sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.


Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.


Farao na afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba.


Ila nchi ya makuhani hakuinunua; maana makuhani walikuwa na posho yao kutoka kwa Farao, wakala posho yao waliyopewa na Farao. Kwa hiyo hawakuuza nchi yao.


Wakasema, Umeyaokoa maisha yetu, na tuone kibali machoni pa bwana wetu, nasi tutakuwa watumwa wa Farao.


Tena tunawaarifu ya kuwa katika habari ya makuhani, na Walawi, na waimbaji, na mabawabu na Wanethini, au watumishi wa nyumba hii ya Mungu, si halali kuwatoza kodi, wala ada, wala ushuru.


Kwa sababu hiyo nitawaleta watu wa mataifa walio wabaya kabisa, nao watazimiliki nyumba zao; tena nitakikomesha kiburi chao wenye nguvu; na mahali pao patakatifu patatiwa unajisi.


Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA.


Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania.


Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika mavuno yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.


Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za mavuno yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo