Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 45:6 - Swahili Revised Union Version

6 Maana miaka hii miwili njaa imekuwa katika nchi, na iko tena miaka mitano isiyo ya kulima wala kuvuna.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Huu ni mwaka wa pili tu wa njaa nchini, na bado kuna miaka mitano zaidi ambapo watu hawataweza kulima wala kuvuna mavuno.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Huu ni mwaka wa pili tu wa njaa nchini, na bado kuna miaka mitano zaidi ambapo watu hawataweza kulima wala kuvuna mavuno.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Huu ni mwaka wa pili tu wa njaa nchini, na bado kuna miaka mitano zaidi ambapo watu hawataweza kulima wala kuvuna mavuno.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Kwa miaka miwili sasa njaa imekuwa katika nchi, pia kwa miaka mitano ijayo hapatakuwa na kulima wala kuvuna.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Kwa miaka miwili sasa imekuwepo njaa katika nchi, pia kwa miaka mitano ijayo hapatakuwepo kulima wala kuvuna.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Maana miaka hii miwili njaa imekuwa katika nchi, na iko tena miaka mitano isiyo ya kulima wala kuvuna.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 45:6
13 Marejeleo ya Msalaba  

Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu, aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu zake; naye alikuwa kijana pamoja na wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akamletea baba yao habari zao mbaya.


Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji.


Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini, aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya uso wa Farao, akasafiri katika nchi yote ya Misri.


Miaka ile saba ya shibe ikaisha katika nchi ya Misri,


ikaanza kuja miaka ile saba ya njaa, kama vile Yusufu alivyosema. Kukawa na njaa katika nchi zote, bali katika nchi yote ya Misri palikuwa na chakula.


Njaa ikawa katika dunia yote pia. Yusufu akazifungua ghala zote, akawauzia Wamisri. Njaa ikawa nzito katika nchi ya Misri.


Na mwaka ule ulipokwisha wakamjia mwaka wa pili, wakamwambia, Hatumfichi bwana wetu ya kwamba fedha zetu zimekwisha, na makundi ya wanyama ni mali ya bwana wetu, hakikusalia kitu mbele za bwana wetu, ila miili yetu na nchi zetu.


Yusufu akawaambia watu, Angalieni, nimewanunua leo, ninyi, na nchi yenu, kuwa mali ya Farao; basi mbegu zenu ni hizi, zipandeni katika nchi.


Utafanya kazi siku sita, lakini katika siku ya saba utapumzika; wakati wa kulima mashamba, na wakati wa kuvuna pia, utapumzika.


Ng'ombe pia na wanapunda wailimao nchi watakula chakula kilichokolea, kilichopepetwa kwa ungo na kwa pepeo.


wazee wa mji huo na wamshushe yule mtamba mpaka bonde lenye maji ya mtoni, lisilolimwa wala kupandwa, wakamvunje yule mtamba shingo yake humo bondeni;


Naye atawaweka kwake kuwa wakuu juu ya maelfu, na makamanda juu ya hamsini hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo