Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Mwanzo 40:7 - Swahili Revised Union Version

7 Akawauliza hao maofisa wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Basi, Yosefu akawauliza maofisa hao wa Farao waliokuwa kifungoni pamoja naye nyumbani mwa bwana wake, “Mbona leo mna nyuso za huzuni?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Basi, Yosefu akawauliza maofisa hao wa Farao waliokuwa kifungoni pamoja naye nyumbani mwa bwana wake, “Mbona leo mna nyuso za huzuni?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Basi, Yosefu akawauliza maofisa hao wa Farao waliokuwa kifungoni pamoja naye nyumbani mwa bwana wake, “Mbona leo mna nyuso za huzuni?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Ndipo Yusufu akawauliza maafisa hao wa Farao waliokuwa chini ya ulinzi pamoja naye nyumbani mwa bwana wake hivi, “Mbona nyuso zenu zimejaa huzuni leo?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Ndipo Yusufu akawauliza maafisa hao wa Farao waliokuwa chini ya ulinzi pamoja naye nyumbani mwa bwana wake, akasema, “Mbona nyuso zenu zimejaa huzuni leo?”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Akawauliza hao maofisa wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo?

Tazama sura Nakili

Mwanzo 40:7
7 Marejeleo ya Msalaba  

Yusufu akawajia asubuhi, akawaona wamefadhaika.

Akawatia wote gerezani siku tatu.

Naye akamwambia, Kwa nini, Ee mwana wa mfalme, unakonda hivi siku kwa siku? Hutaki kuniambia? Amnoni akamwambia, Nampenda Tamari, dada ya kaka yangu, Absalomu.

Basi mfalme akaniambia, Mbona umesikitika uso wako, nawe huna ugonjwa? Nini hii, isipokuwa ni huzuni ya moyo? Ndipo nikaogopa sana.

Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao.

Akasema, Ninyi mmeichukua miungu niliyoifanya, na huyo kuhani, nanyi mmekwenda zenu, nami nina nini tena? Basi imekuwaje ninyi kuniuliza, Una nini wewe?

Elkana mumewe akamwambia, Hana, unalilia nini? Kwa nini huli? Kwa nini moyo wako una huzuni? Je! Mimi si bora kwako kuliko watoto kumi?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo