Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 33:18 - Swahili Revised Union Version

18 Yakobo akaja kwa amani mpaka katika mji wa Shekemu, ulio katika nchi ya Kanaani, alipokuja kutoka Padan-aramu; akapiga kambi mbele ya huo mji.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Kutoka Padan-aramu, Yakobo alifika salama mjini Shekemu, katika nchi ya Kanaani, akapiga kambi yake karibu na mji huo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Kutoka Padan-aramu, Yakobo alifika salama mjini Shekemu, katika nchi ya Kanaani, akapiga kambi yake karibu na mji huo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Kutoka Padan-aramu, Yakobo alifika salama mjini Shekemu, katika nchi ya Kanaani, akapiga kambi yake karibu na mji huo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Baada ya Yakobo kutoka Padan-Aramu, alifika salama katika mji wa Shekemu huko Kanaani, na kuweka kambi yake karibu na mji huo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Baada ya Yakobo kutoka Padan-Aramu, alifika salama katika mji wa Shekemu huko Kanaani na kuweka kambi yake karibu na mji.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

18 Yakobo akaja kwa amani mpaka katika mji wa Shekemu, ulio katika nchi ya Kanaani, alipokuja kutoka Padan-aramu; akapiga kambi mbele ya huo mji.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 33:18
16 Marejeleo ya Msalaba  

Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo.


Isaka akawa mwenye miaka arubaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake.


Ondoka, uende Padan-aramu, mpaka nyumba ya Bethueli baba ya mama yako, ukajitwalie huko mke katika binti za Labani, ndugu wa mama yako.


Labani akamfikia Yakobo, na Yakobo alikuwa amepiga hema zake katika mlima, na Labani na ndugu zake wakapiga hema zao katika nchi ya milima ya Gileadi.


Mungu akamtokea Yakobo tena, aliporudi kutoka Padan-aramu akambariki.


Israeli akamwambia Yusufu, Je! Ndugu zako hawachungi kondoo katika Shekemu? Njoo, nikutume kwao. Akamwambia, Mimi hapa.


Hao ndio wana wa Lea, aliomzalia Yakobo katika Padan-aramu, na Dina, binti yake. Wanawe wote wa kiume na kike walikuwa watu thelathini na watatu.


Na mimi nilipokuja kutoka Padan, Raheli akanifia katika nchi ya Kanaani, njiani, si mwendo mkubwa kabla ya kufika Efrata. Nikamzika katika njia ya Efrata, ndio Bethlehemu.


Mungu amenena kwa utakatifu wake, Nami nikishangilia. Nitaigawanya Shekemu, Na kulipima bonde la Sukothi.


wakafika watu kadhaa toka Shekemu, na toka Shilo, na toka Samaria, watu themanini, nao wamenyoa ndevu zao, na kurarua nguo zao, nao wamejikatakata, wakichukua sadaka na ubani mikononi mwao, ili wazilete nyumbani kwa BWANA.


Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa.


Basi akafika katika mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe.


wakachukuliwa mpaka Shekemu wakazikwa katika kaburi lile, ambalo Abrahamu alilinunua kwa kima fulani cha fedha kutoka kwa wana wa Hamori, huko Shekemu.


Yoshua akawakusanya makabila yote ya Israeli huko Shekemu, akawaita wazee wa Israeli, na wakuu wao, na waamuzi wao, na maofisa wao nao wakaja mbele za Mungu.


Abimeleki, mwana wa Yerubaali, akaenda Shekemu kwa ndugu za mama yake, akanena nao, na wote waliokuwa wa nyumba ya baba ya mama yake, akasema,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo