Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Mwanzo 27:19 - Swahili Revised Union Version

19 Yakobo akamwambia babaye, Mimi ni Esau, mzaliwa wako wa kwanza, nimefanya kama ulivyoniambia. Inuka, tafadhali, ukae kitako, ule mawindo yangu, ili roho yako inibariki.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Yakobo akamjibu baba yake, “Ni mimi Esau, mzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniagiza. Tafadhali baba, kaa kitako ule mawindo yangu ili upate kunibariki.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Yakobo akamjibu baba yake, “Ni mimi Esau, mzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniagiza. Tafadhali baba, kaa kitako ule mawindo yangu ili upate kunibariki.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Yakobo akamjibu baba yake, “Ni mimi Esau, mzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniagiza. Tafadhali baba, kaa kitako ule mawindo yangu ili upate kunibariki.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Yakobo akamwambia baba yake, “Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniambia. Tafadhali uketi, ule sehemu ya mawindo yangu ili unibariki.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Yakobo akamwambia baba yake, “Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniambia. Tafadhali uketi, ule sehemu ya mawindo yangu ili uweze kunibariki.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

19 Yakobo akamwambia babaye, Mimi ni Esau, mzaliwa wako wa kwanza, nimefanya kama ulivyoniambia. Inuka, tafadhali, ukae kitako, ule mawindo yangu, ili roho yako inibariki.

Tazama sura Nakili

Mwanzo 27:19
15 Marejeleo ya Msalaba  

Wa kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau.

Basi Isaka akampenda Esau, kwa sababu alikula mawindo yake, na Rebeka akampenda Yakobo.

Akaja kwa baba yake, akasema, Babangu. Akasema, Mimi hapa, U nani wewe, mwanangu?

Isaka akamwambia Yakobo, Karibu, tafadhali, ili nikupapase, mwanangu, nione kwamba wewe ndiwe mwanangu Esau, ama siyo.

Naye pia amefanya chakula kitamu akamletea babaye, akamwambia baba yake. Babangu na ainuke, ale mawindo ya mwanawe, ili uweze kunibariki.

Akasema, Nduguyo amekuja kwa hila, akaichukua baraka yako.

ukaniandalie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa.

hadi ikuondokee ghadhabu ya ndugu yako, akasahau uliyomtenda. Ndipo nitakapotuma watu kukuchukua kutoka huko. Kwa nini nifiwe nanyi nyote wawili siku moja?

Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la BWANA, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.

Yeroboamu akamwambia mkewe, Ondoka, tafadhali, ujibadilishe, wasikujue kuwa mkewe Yeroboamu; ukaende Shilo; tazama, yuko huko Ahiya nabii, aliyeninena mimi ya kwamba nitakuwa mfalme juu ya watu hawa.

Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo