Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 20:12 - Swahili Revised Union Version

12 Hata hivyo, kwa kweli yeye ni dada yangu, yaani binti wa baba yangu na wala sio binti wa mama yangu; ndipo akawa mke wangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Zaidi ya hayo, kwa kweli, yeye ni dada yangu: Baba yake na baba yangu ni mmoja, lakini mama tofauti; ndiyo maana akawa mke wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Zaidi ya hayo, kwa kweli, yeye ni dada yangu: Baba yake na baba yangu ni mmoja, lakini mama tofauti; ndiyo maana akawa mke wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Zaidi ya hayo, kwa kweli, yeye ni dada yangu: baba yake na baba yangu ni mmoja, lakini mama tofauti; ndiyo maana akawa mke wangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti ya baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti wa baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 Hata hivyo, kwa kweli yeye ni dada yangu, yaani binti wa baba yangu na wala sio binti wa mama yangu; ndipo akawa mke wangu.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 20:12
8 Marejeleo ya Msalaba  

Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska.


Tafadhali useme, wewe u ndugu yangu, iwe heri kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu iishi kwa ajili yako.


Abrahamu akasema, Kwa kuwa niliona, hakika hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu.


Ikawa hapo Mungu aliponisafirisha kutoka nyumba ya baba yangu, nikamwambia, Hii ndiyo fadhili yako, utakayonifanyia. Kila mahali tuingiapo, useme, Huyu ni kaka yangu.


Abrahamu akanena juu ya Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu”. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma watu wakamtwaa Sara.


Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni dada yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso.


Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa.


jitengeni na ubaya wa kila namna.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo