Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 13:8 - Swahili Revised Union Version

8 Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu jamaa moja.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Basi, Abramu akamwambia Loti, “Kusiwe na mafarakano kati yetu wala kati ya wachungaji wako na wachungaji wangu, kwa sababu sisi ni jamaa moja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Basi, Abramu akamwambia Loti, “Kusiwe na mafarakano kati yetu wala kati ya wachungaji wako na wachungaji wangu, kwa sababu sisi ni jamaa moja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Basi, Abramu akamwambia Loti, “Kusiwe na mafarakano kati yetu wala kati ya wachungaji wako na wachungaji wangu, kwa sababu sisi ni jamaa moja.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Hivyo Abramu akamwambia Lutu, “Pasiwe na ugomvi wowote kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wako, kwa kuwa sisi ni ndugu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Hivyo Abramu akamwambia Lutu, “Pasiwe na ugomvi wowote kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wako, kwa kuwa sisi ni ndugu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu jamaa moja.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 13:8
30 Marejeleo ya Msalaba  

Je! Nchi hii yote haiko mbele yako? Basi jitenge nami, nakusihi; ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kulia; ukienda upande wa kulia, nitakwenda upande wa kushoto.


Abramu aliposikia ya kwamba nduguye amechukuliwa mateka, akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata mpaka Dani.


Akaagana na ndugu zake, wakaenda zao; naye akawaambia, Msigombane njiani.


Semeni, Watumishi wako tumekuwa wachunga wanyama tangu ujana wetu, na hata leo, sisi, na baba zetu; mpate kukaa katika nchi ya Gosheni; maana kila mchunga wanyama ni chukizo kwa Wamisri.


Tazama, jinsi ilivyo vyema, na kupendeza, Ndugu kuishi pamoja, kwa umoja.


Akatoka siku ya pili, na tazama, watu wawili wa Waebrania walikuwa wakipigana. Akamwambia yule aliyemdhulumu mwenzake, Mbona unampiga mwenzako?


Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.


Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.


Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake; Bali kila mpumbavu ataka kugombana.


Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.


Kesho yake akawatokea walipokuwa wakishindana, akataka kuwapatanisha, akisema, Enyi bwana zangu, ninyi ni ndugu. Mbona mnadhulumiana?


Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;


Yatendeni mambo yote pasipo manung'uniko wala mashindano,


Kuhusu upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.


Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;


Upendano wa ndugu na udumu.


Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo safi.


Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.


Neno la mwisho ni hili; muwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;


Zaidi ya yote iweni na bidii kubwa katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.


na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.


Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.


Kisha Gaali, mwana wa Ebedi, akaenda pamoja na nduguze, wakavuka na kufika Shekemu; na watu wa Shekemu wakawa na imani naye.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo