Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mhubiri 8:14 - Swahili Revised Union Version

14 Kuna ubatili unaofanyika juu ya nchi, kwamba wako wenye haki nao wapatilizwa kama kwa kazi yao waovu; tena wako waovu, nao wapatilizwa kama kwa kazi yao wenye haki. Nami nikasema ya kuwa hayo nayo ni ubatili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Kuna jambo moja, bure kabisa nililoligundua hapa duniani: Watu wema hutendewa wastahilivyo waovu, nao waovu hutendewa wastahilivyo watu wema. Hili nalo nasema ni bure kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Kuna jambo moja, bure kabisa nililoligundua hapa duniani: Watu wema hutendewa wastahilivyo waovu, nao waovu hutendewa wastahilivyo watu wema. Hili nalo nasema ni bure kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Kuna jambo moja, bure kabisa nililoligundua hapa duniani: watu wema hutendewa wastahilivyo waovu, nao waovu hutendewa wastahilivyo watu wema. Hili nalo nasema ni bure kabisa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kuna kitu kingine ambacho ni ubatili kinachofanyika duniani: Watu waadilifu kupata yale yanayowastahili waovu, nao waovu kupata yale yanayowastahili waadilifu. Hili nalo pia, nasema ni ubatili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kuna kitu kingine ambacho ni ubatili kinachotokea duniani: Watu waadilifu kupata yale yanayowastahili waovu, nao waovu kupata yale yanayowastahili waadilifu. Hili nalo pia, nasema ni ubatili.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Kuna ubatili unaofanyika juu ya nchi, kwamba wako wenye haki nao wapatilizwa kama kwa kazi yao waovu; tena wako waovu, nao wapatilizwa kama kwa kazi yao wenye haki. Nami nikasema ya kuwa hayo nayo ni ubatili.

Tazama sura Nakili




Mhubiri 8:14
16 Marejeleo ya Msalaba  

Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu.


Mbona waovu wanaishi, Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu?


Tazama, ninyi nyote mmeyaona wenyewe; Mbona basi mmebatilika kabisa?


Maana niliwaonea wivu wenye kujivuna, Nilipoiona hali ya amani ya wasio haki.


Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye;


macho yake mwenye hekima yamo kichwani mwake, lakini mpumbavu huenda gizani; ila hata hivyo nikatambua ya kwamba ni tukio moja la mwisho liwapatalo wote sawasawa.


Tena nikagundua kuwa juhudi zote, na ustadi wote katika kazi, hutokana na mtu kumwonea mwingine wivu. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.


Kuna mtu aliye peke yake, wala hana mwenzi wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.


Mambo hayo yote nimeyaona mimi katika siku za ubatili wangu, yuko mwenye haki apoteaye katika haki yake, yuko na mtu mwovu azidishaye maisha yake katika udhalimu wake.


Wewe u mwenye haki, Ee BWANA, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki. Mbona njia ya wabaya inasitawi? Mbona wote watendao hila wanakaa salama?


Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo