Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 21:31 - Swahili Revised Union Version

31 Farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita; Lakini BWANA ndiye aletaye wokovu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Farasi hutayarishwa kwa vita, lakini ushindi wamtegemea Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Farasi hutayarishwa kwa vita, lakini ushindi wamtegemea Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Farasi hutayarishwa kwa vita, lakini ushindi wamtegemea Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita, bali ushindi huwa kwa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita, bali ushindi huwa kwa bwana.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

31 Farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita; Lakini BWANA ndiye aletaye wokovu.

Tazama sura Nakili




Methali 21:31
13 Marejeleo ya Msalaba  

ila huyo alisimama katikati ya konde lile, akalipigania, akawaua Wafilisti; naye BWANA akafanya wokovu mkuu.


Awapaye wafalme wokovu, Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu.


Hapendezwi na nguvu za farasi, Wala hairidhii miguu ya mkimbiaji.


Hawa wanataja magari na hawa farasi, Lakini sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.


Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.


Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.


Wokovu ni wa BWANA; Baraka yako na iwe juu ya watu wako.


Mungu wetu ni Mungu wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana.


Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.


Ole wao wateremkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti BWANA!


Ni kweli, msaada haufai unaotazamiwa kutoka milimani, makutano yenye mshindo juu ya milima; ni kweli, wokovu wa Israeli ni katika BWANA, Mungu wetu.


Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo