Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 5:33 - Swahili Revised Union Version

33 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana viapo vyako;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 “Tena mmesikia kwamba watu wa kale waliambiwa: ‘Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 “Tena mmesikia kwamba watu wa kale waliambiwa: ‘Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 “Tena mmesikia kwamba watu wa kale waliambiwa: ‘Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 “Tena mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiape kwa uongo, bali timiza kiapo kile ulichofanya kwa Mwenyezi Mungu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 “Tena mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiape kwa uongo, bali timiza kiapo kile ulichofanya kwa Bwana Mwenyezi Mungu.’

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

33 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana viapo vyako;

Tazama sura Nakili




Mathayo 5:33
15 Marejeleo ya Msalaba  

Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye Juu nadhiri zako.


Wekeni nadhiri na mziondoe Kwa BWANA, Mungu wenu. Wote wanaomzunguka wamletee hedaya, Yeye astahiliye kuogopwa.


Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.


Msiape uongo kwa jina langu, na ukalinajisi jina la Mungu wako; Mimi ndimi BWANA.


Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.


Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.


Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;


Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.


Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri BWANA, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako.


Usilitaje bure Jina la BWANA, Mungu wako; maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia, mtu alitajaye jina lake bure.


Mche BWANA, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake.


na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na linginelo lolote lisilopatana na mafundisho ya kweli;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo