Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 25:14 - Swahili Revised Union Version

14 Maana itakuwa kama mfano wa mtu aliyetaka kusafiri, akawaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 “Wakati huo itakuwa kama mtu mmoja aliyetaka kusafiri ngambo: Aliwaita watumishi wake, akawakabidhi mali yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 “Wakati huo itakuwa kama mtu mmoja aliyetaka kusafiri ngambo: Aliwaita watumishi wake, akawakabidhi mali yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 “Wakati huo itakuwa kama mtu mmoja aliyetaka kusafiri ng'ambo: aliwaita watumishi wake, akawakabidhi mali yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 “Tena, ufalme wa mbinguni ni kama mtu aliyetaka kusafiri, naye akawaita watumishi wake na kuweka mali yake kwenye uangalizi wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 “Tena, Ufalme wa Mbinguni ni kama mtu aliyetaka kusafiri, naye akawaita watumishi wake na kuweka mali yake kwenye uangalizi wao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Maana itakuwa kama mfano wa mtu aliyetaka kusafiri, akawaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.

Tazama sura Nakili




Mathayo 25:14
13 Marejeleo ya Msalaba  

Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye shamba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia ua, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.


Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.


Akaanza kuwaambia watu mfano huu; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu; akakondisha wakulima, akaenda akakaa katika nchi nyingine muda mrefu.


Basi kuna karama tofauti; bali Roho ni yeye yule.


Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa.


Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo