Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Matendo 28:18 - Swahili Revised Union Version

18 Na hao walipokwisha kunihoji walitaka kunifungua, kwa maana hapakuwa na sababu yoyote kwangu ya kuuawa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Waliponihoji na kuona kwamba sikuwa na hatia yoyote, walitaka kuniachia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Waliponihoji na kuona kwamba sikuwa na hatia yoyote, walitaka kuniachia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Waliponihoji na kuona kwamba sikuwa na hatia yoyote, walitaka kuniachia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Wao walipokwisha kunihoji, wakataka kuniachia huru kwa sababu hawakuona kosa lolote nililolifanya linalostahili adhabu ya kifo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Wao walipokwisha kunihoji, wakataka kuniachia huru kwa sababu hawakuona kosa lolote nililolifanya linalostahili adhabu ya kifo.

Tazama sura Nakili

Matendo 28:18
8 Marejeleo ya Msalaba  

Kesho yake akitaka kujua hakika, ni kwa sababu gani ameshitakiwa na Wayahudi, akamfungua, akawaamuru wakuu wa makuhani na baraza yote wakutane. Akamleta Paulo chini, akamweka mbele yao.

nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lolote la kustahili kuuawa wala kufungwa.

Na mtawala alipompungia mkono ili anene, Paulo akajibu, Kwa kuwa ninajua ya kwamba wewe umekuwa mwamuzi wa taifa hili kwa muda wa miaka mingi, najitetea mwenyewe kwa moyo wa furaha.

Basi Feliki aliwaahirisha, kwa sababu alijua habari za Njia ile kwa usahihi zaidi, akasema, Lisia jemadari atakapoteremka nitaamua kesi yenu.

Lakini mimi niliona kwamba hakutenda neno la kustahili kuuawa, na yeye mwenyewe alipotaka kuhukumiwa na Kaisari, nilikusudia kumpeleka kwake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo