Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Matendo 24:8 - Swahili Revised Union Version

8 Akawaamuru wale waliomshitaki waje kwako.] Wewe mwenyewe kwa kumwulizauliza utaweza kupata habari ya mambo yale yote tunayomshitaki sisi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Kisha akaamuru washtaki wake waje mbele yako.] Kama ukimhoji wewe mwenyewe, utaweza kubainisha mambo haya yote tunayomshtaki kwayo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Kisha akaamuru washtaki wake waje mbele yako.] Kama ukimhoji wewe mwenyewe, utaweza kubainisha mambo haya yote tunayomshtaki kwayo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Kama ukimhoji wewe mwenyewe, utaweza kubainisha mambo haya yote tunayomshtaki kwayo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 akiwaamuru washtaki wake waje mbele yako.] Kwa kumchunguza mwenyewe utaweza kujua ukweli kuhusu mashtaka haya yote tunayoleta dhidi yake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 akiwaamuru washtaki wake waje mbele yako: ili] kwa kumchunguza wewe mwenyewe unaweza kujua kutoka kwake mambo yote tunayomshtaki kwayo.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Akawaamuru wale waliomshitaki waje kwako.] Wewe mwenyewe kwa kumwulizauliza utaweza kupata habari ya mambo yale yote tunayomshitaki sisi.

Tazama sura Nakili




Matendo 24:8
7 Marejeleo ya Msalaba  

akawaambia, Mtu huyu mmemleta kwangu kana kwamba anapotosha watu; nami, tazama, nimeamua mambo yake mbele yenu, ila sikuona kwake kosa lolote katika mambo hayo mliyomshitaki;


Hata nilipopewa habari kwamba patakuwa na ghasia juu ya mtu huyu, mara nikamtuma kwako, nikawaagiza na wale waliomshitaki, wanene habari zake mbele yako. Wasalamu.


akasema, Nitakusikia wewe watakapokuja wale waliokushitaki; akaamuru alindwe katika nyumba ya utawala wa Herode.


Lakini Lisia jemadari akafika akamwondoa mikononi mwetu kwa nguvu,


Wayahudi nao wakamshitaki, wakisema ya kuwa ndivyo yalivyo.


Akasema, Wale walio na mamlaka kwenu na wateremke pamoja nami wakamshitaki, ikiwa liko neno baya katika mtu huyu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo