Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Matendo 20:25 - Swahili Revised Union Version

25 Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huku na huko, hamtaniona uso tena.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 “Nimepita miongoni mwenu nyote nikiuhubiri ufalme wa Mungu. Sasa lakini, najua hakuna hata mmoja wenu atakayeniona tena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 “Nimepita miongoni mwenu nyote nikiuhubiri ufalme wa Mungu. Sasa lakini, najua hakuna hata mmoja wenu atakayeniona tena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 “Nimepita miongoni mwenu nyote nikiuhubiri ufalme wa Mungu. Sasa lakini, najua hakuna hata mmoja wenu atakayeniona tena.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 “Nami sasa najua kuwa hakuna hata mmoja miongoni mwenu niliowahubiria ufalme wa Mungu atakayeniona tena.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 “Nami sasa najua ya kuwa hakuna hata mmoja miongoni mwenu ambaye nimemhubiria Ufalme wa Mwenyezi Mungu katika kwenda kwangu huku na huko, atakayeniona uso tena.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

25 Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huku na huko, hamtaniona uso tena.

Tazama sura Nakili




Matendo 20:25
13 Marejeleo ya Msalaba  

Na katika kuenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.


Kila mtu alisikiapo neno la ufalme bila kulielewa, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.


Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.


Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila namna waliyokuwa nayo watu.


Torati na Manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo Habari Njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu.


Akamwambia Waache wafu wawazike wafu wao; bali wewe nenda ukautangaze ufalme wa Mungu.


wakihuzunika zaidi kwa sababu ya neno lile alilosema, ya kwamba hawatamwona uso tena. Wakamsindikiza hata merikebuni.


akihubiri habari za ufalme wa Mungu, na kuyafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu.


Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri Habari Njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.


Lakini sasa, kwa kuwa sina wasaa tena pande hizi, tena kwa miaka mingi nimekuwa nikitamani kuja kwenu;


Lakini sikujulikana uso wangu na makanisa ya Yudea yaliyokuwa katika Kristo;


Maana nataka ninyi mjue jinsi ilivyo kuu juhudi yangu niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo