Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Matendo 19:32 - Swahili Revised Union Version

32 Basi wengine walikuwa wakilia hivi na wengine hivi; kwa maana ule mkutano ulikuwa umechafukachafuka, na wengi wao hawakuijua sababu ya kukusanyika kwao pamoja.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Wakati huo, kila mtu alikuwa anapayuka; wengine hili na wengine lile, mpaka hata ule mkutano ukavurugika. Wengi hawakujua hata sababu ya kukutana kwao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Wakati huo, kila mtu alikuwa anapayuka; wengine hili na wengine lile, mpaka hata ule mkutano ukavurugika. Wengi hawakujua hata sababu ya kukutana kwao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Wakati huo, kila mtu alikuwa anapayuka; wengine hili na wengine lile, mpaka hata ule mkutano ukavurugika. Wengi hawakujua hata sababu ya kukutana kwao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Umati wa watu walikuwa na taharuki. Walikuwa wakipiga kelele, hawa wakisema hili na wengine lile. Idadi kubwa ya watu hawakujua hata ni kwa nini walikuwa wamekusanyika huko.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Ule umati ulikuwa na taharuki. Wengine walikuwa wakipiga kelele, hawa wakisema hili na wengine lile. Idadi kubwa ya watu hawakujua hata ni kwa nini walikuwa wamekusanyika huko.

Tazama sura Nakili




Matendo 19:32
6 Marejeleo ya Msalaba  

Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia ukumbi wa michezo kwa pamoja, wakiisha kuwakamata Gayo na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paulo.


Na baadhi ya wakuu wa Asia, walio rafiki zake, wakatuma watu kwake, wakimsihi asiingie ndani katika ukumbi wa michezo.


Kwa maana tuna hatari ya kushitakiwa kwa ajili ya ghasia hizi za leo, ambazo hazina sababu; maana hakuna sababu tunayoweza kutoa kama chanzo cha ghasia hizi.


Wengine katika makutano wakapiga kelele wakisema hivi, na wengine hivi. Basi alipokuwa hawezi kupata hakika ya habari kwa sababu ya zile kelele, akatoa amri aletwe ndani ya ngome.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo