Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Matendo 16:35 - Swahili Revised Union Version

35 Kulipopambazuka mahakimu wakawatuma wakubwa wa askari wakisema, Waacheni watu wale waende zao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Kesho yake asubuhi, mahakimu waliwatuma maofisa wao wakisema, “Wafungueni wale watu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 Kesho yake asubuhi, mahakimu waliwatuma maofisa wao wakisema, “Wafungueni wale watu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Kesho yake asubuhi, mahakimu waliwatuma maofisa wao wakisema, “Wafungueni wale watu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Kulipopambazuka wale mahakimu wakawatuma maafisa wao kwa mkuu wa gereza wakiwa na agizo linalosema, “Wafungue wale watu, waachie waende zao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Kulipopambazuka wale mahakimu wakawatuma maafisa wao kwa mkuu wa gereza wakiwa na agizo linalosema, “Wafungue wale watu, waache waende zao.”

Tazama sura Nakili




Matendo 16:35
9 Marejeleo ya Msalaba  

Maana hasira ya binadamu itakusifu, Masalio ya hasira utajifunga kama mshipi.


Je! Hamniogopi mimi? Asema BWANA; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.


Na watakapowapeleka ninyi mbele ya masinagogi na watawala na wenye mamlaka, msifadhaike kwa kuwaza maneno yenu jinsi mtakavyojibu au kusema;


Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu.


Yule mlinzi wa gereza akamwarifu Paulo maneno haya akisema, Mahakimu wametuma watu ili mfunguliwe; basi, sasa tokeni nje, nendeni zenu kwa amani.


Wakubwa wa askari wakawaambia mahakimu maneno haya; nao wakaogopa, waliposikia ya kwamba hao ni Warumi.


Nao walipokwisha kuwatisha tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu; kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka;


Wakakubali maneno yake; nao walipowaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kisha wakawaacha waende zao.


Basi Yoshua akawaamuru hao makuhani, akawaambia, Haya, kweeni mtoke Yordani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo