Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Marko 14:61 - Swahili Revised Union Version

61 Lakini akanyamaza, wala hakujibu neno. Kuhani Mkuu akamwuliza tena, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mtukufu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

61 Lakini yeye akakaa kimya; hakusema hata neno moja. Kuhani mkuu akamwuliza tena, “Je, wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu Mtukufu?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

61 Lakini yeye akakaa kimya; hakusema hata neno moja. Kuhani mkuu akamwuliza tena, “Je, wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu Mtukufu?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

61 Lakini yeye akakaa kimya; hakusema hata neno moja. Kuhani mkuu akamwuliza tena, “Je, wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu Mtukufu?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

61 Lakini Isa akakaa kimya, hakusema neno lolote. Kuhani mkuu akamuuliza tena, “Je, wewe ndiwe Al-Masihi, Mwana wa Mungu Aliyebarikiwa?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

61 Lakini Isa akakaa kimya, hakusema neno lolote. Kuhani mkuu akamuuliza tena, “Je, wewe ndiwe Al-Masihi, Mwana wa Mwenyezi Mungu Aliyebarikiwa?”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

61 Lakini akanyamaza, wala hakujibu neno. Kuhani Mkuu akamwuliza tena, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mtukufu?

Tazama sura Nakili




Marko 14:61
30 Marejeleo ya Msalaba  

Ee BWANA, umehimidiwa, Unifundishe amri zako.


Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia, Wewe ni mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.


Nimenyamaza, sifumbui kinywa changu, Maana Wewe ndiwe uliyeyafanya.


Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.


Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.


na tazama, sauti kutoka mbinguni ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.


Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya wakati wetu?


Kisha Kuhani Mkuu akasimama katikati, akamwuliza Yesu, akisema, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini?


Pilato akamwuliza, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu, akamwambia, Wewe wasema.


Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.


Basi Wayahudi walimzunguka, wakamwambia, Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi.


je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nilisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?


Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nilikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.


Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu.


Akaingia tena ndani ya ile Praitorio, akamwambia Yesu, Wewe umetoka wapi? Lakini Yesu hakumpa jibu lolote.


Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake yule amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.


kama ilivyonenwa katika Habari Njema ya utukufu wa Mungu ahimidiwaye, niliyowekewa amana.


ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana;


Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo