Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Marko 12:32 - Swahili Revised Union Version

32 Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Basi, yule mwalimu wa sheria akamwambia, “Vyema Mwalimu! Umesema ukweli kwamba Mungu ni mmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Basi, yule mwalimu wa sheria akamwambia, “Vyema Mwalimu! Umesema ukweli kwamba Mungu ni mmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Basi, yule mwalimu wa sheria akamwambia, “Vyema Mwalimu! Umesema ukweli kwamba Mungu ni mmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Yule mwalimu wa Torati akamwambia Isa, “Mwalimu, umejibu vyema kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Yule mwalimu wa Torati akamwambia Isa, “Mwalimu, umejibu vyema kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

32 Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye;

Tazama sura Nakili

Marko 12:32
13 Marejeleo ya Msalaba  

Msiogope wala msifanye hofu; je! Sikukuambia haya zamani na kuyatangaza? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine.

BWANA asema hivi, Kazi ya Misri, na bidhaa ya Kushi, na Waseba, watu walio warefu, watakujia, nao watakuwa wako; watakufuata; watakuja katika minyororo; wataanguka chini mbele yako, watakuomba, wakisema, Hakika Mungu yu ndani yako; wala hapana mwingine, hapana Mungu tena.

Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba iwe ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.

kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi;

Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;

na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhabihu zote pia.

Wewe umeoneshwa haya, ili upate kujua ya kuwa BWANA ndiye Mungu, hapana mwingine ila yeye.

Kwa hiyo ujue, leo hivi, ukaweke moyoni mwako, ya kuwa BWANA ndiye Mungu katika mbingu juu, na katika nchi chini; hapana mwingine.

Usiwe na miungu mingine ila mimi.

Sikiliza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja

Tufuate:

Matangazo

Matangazo