Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Maombolezo 2:8 - Swahili Revised Union Version

8 BWANA amekusudia kuuharibu Ukuta wa binti Sayuni; Ameinyosha hiyo kamba, Hakuuzuia mkono wake usiangamize; Bali amefanya boma na ukuta kuomboleza; Zote pamoja hudhoofika.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Mwenyezi-Mungu alipania kuubomoa ukuta wa mji wa Siyoni; aliupima na kuhakikisha kila kitu kimeharibiwa; minara na kuta za nje ya mji akazifanya ukiwa, zote kwa pamoja zikaangamia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Mwenyezi-Mungu alipania kuubomoa ukuta wa mji wa Siyoni; aliupima na kuhakikisha kila kitu kimeharibiwa; minara na kuta za nje ya mji akazifanya ukiwa, zote kwa pamoja zikaangamia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Mwenyezi-Mungu alipania kuubomoa ukuta wa mji wa Siyoni; aliupima na kuhakikisha kila kitu kimeharibiwa; minara na kuta za nje ya mji akazifanya ukiwa, zote kwa pamoja zikaangamia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Mwenyezi Mungu alikusudia kuangusha ukuta uliomzunguka Binti Sayuni. Ameinyoosha kamba ya kupimia na hakuuzuia mkono wake usiangamize. Alifanya maboma na kuta ziomboleze, vyote vikaharibika pamoja.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 bwana alikusudia kuangusha ukuta uliomzunguka Binti Sayuni. Ameinyoosha kamba ya kupimia na hakuuzuia mkono wake usiangamize. Alifanya maboma na kuta ziomboleze, vyote vikaharibika pamoja.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 BWANA amekusudia kuuharibu Ukuta wa binti Sayuni; Ameinyosha hiyo kamba, Hakuuzuia mkono wake usiangamize; Bali amefanya boma na ukuta kuomboleza; Zote pamoja hudhoofika.

Tazama sura Nakili




Maombolezo 2:8
17 Marejeleo ya Msalaba  

Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba wakiwa wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi.


Nami nitanyosha juu ya Yerusalemu kamba ya Samaria, na timazi ya nyumba ya Ahabu; nami nitaifuta Yerusalemu, kama mtu afutavyo sahani, kuifuta na kuifudikiza.


Uondoe mkono wako usinilemee; Na utisho wako usinitie hofu.


Kwa maana siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa, siku ya fujo inakuja, itokayo kwa Bwana, BWANA wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima.


Nami nitafanya hukumu kuwa ndiyo kanuni, na haki kuwa ndiyo timazi; na mvua ya mawe itachukulia mbali hilo kimbilio la maneno ya uongo, na maji yatapagharikisha mahali pa kujisitiri.


Na malango yake yatalia na kuomboleza, naye atakuwa ukiwa, atakaa chini.


Kozi na nungunungu wataimiliki, bundi na kunguru watakaa huko, naye atanyosha juu yake kamba ya ukiwa na timazi ya utupu.


Haya basi, sasa nitawaambieni nitakalolitenda shamba langu la mizabibu; nitaondoa ua wake, nalo litaliwa; nitabomoa ukuta wake, nalo litakanyagwa;


Yuda huomboleza, Na malango yake yamelegea; Wameketi chini wamevaa kaniki; Na kilio cha Yerusalemu kimepaa juu.


Pandeni juu ya kuta zake mkaharibu, lakini msiharibu kabisa; ondoeni matawi yake; kwa maana si yake BWANA.


Akaiteketeza nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto.


BWANA ameyatenda aliyoyakusudia; amelitimiza neno lake, Aliloliamuru siku za kale; Ameangusha hata chini, Wala hakuona huruma; Naye amemfurahisha adui juu yako, Ameitukuza pembe ya watesi wako.


Mioyo yao ilimlilia Bwana; Ee ukuta wa binti Sayuni! Machozi na yachuruzike kama mto Mchana na usiku; Usijipatie kupumzika; Mboni ya jicho lako isikome.


Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo, Wala hakuona huruma; Ameziangusha ngome za binti Yuda Katika ghadhabu yake; Amezibomoa hata nchi Ameunajisi ufalme na wakuu wake.


Bwana amekuwa mfano wa adui, Amemmeza Israeli; Ameyameza majumba yake yote, Ameziharibu ngome zake; Tena amemzidishia binti Yuda Matanga na maombolezo.


Lakini niliuzuia mkono wangu, nikatenda kwa ajili ya jina langu, lisitiwe unajisi mbele ya macho ya mataifa, ambao mbele ya macho yao niliwatoa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo