Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Maombolezo 2:6 - Swahili Revised Union Version

6 Naye ameondoa maskani yake kwa nguvu, Kana kwamba ni ya bustani tu; Ameziharibu sikukuu zake; BWANA amezisahaulisha katika Sayuni Sikukuu na sabato; Naye amewadharau mfalme na kuhani Katika uchungu wa hasira yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Hekalu lake amelibomoa kama kitalu bustanini, maskani yake ameiharibu. Amefutilia mbali sikukuu na Sabato huko Siyoni, kwa hasira yake kuu amewakataa mfalme na makuhani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Hekalu lake amelibomoa kama kitalu bustanini, maskani yake ameiharibu. Amefutilia mbali sikukuu na Sabato huko Siyoni, kwa hasira yake kuu amewakataa mfalme na makuhani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Hekalu lake amelibomoa kama kitalu bustanini, maskani yake ameiharibu. Amefutilia mbali sikukuu na Sabato huko Siyoni, kwa hasira yake kuu amewakataa mfalme na makuhani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Ameharibu maskani yake kama bustani, ameharibu mahali pake pa mkutano. Mwenyezi Mungu amemfanya Sayuni kusahau sikukuu zake zilizoamriwa na Sabato zake; katika hasira yake kali amewadharau mfalme na kuhani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Ameharibu maskani yake kama bustani, ameharibu mahali pake pa mkutano. bwana amemfanya Sayuni kusahau sikukuu zake zilizoamriwa na Sabato zake; katika hasira yake kali amewadharau mfalme na kuhani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Naye ameondoa maskani yake kwa nguvu, Kana kwamba ni ya bustani tu; Ameziharibu sikukuu zake; BWANA amezisahaulisha katika Sayuni Sikukuu na sabato; Naye amewadharau mfalme na kuhani Katika uchungu wa hasira yake.

Tazama sura Nakili




Maombolezo 2:6
25 Marejeleo ya Msalaba  

Wamepatia moto patakatifu pako; Wamelinajisi kao la jina lako hata chini.


Kibanda chake pia kiko Salemu, Na maskani yake iko Sayuni.


Kwa nini umezibomoa kuta zake, Wakauchuma wote wapitao njiani?


Umeyabomoa maboma yake yote, Umezifanya ngome zake kuwa magofu.


Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mwandamo na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada.


Na binti Sayuni ameachwa kama kibanda katika shamba la mizabibu, kama kipenu katika shamba la matango, kama mji uliohusuriwa.


Kwa hiyo nitawatia unajisi wakuu wa patakatifu, nami nitamfanya Yakobo kuwalaani, na Israeli kuwa tukano.


Haya basi, sasa nitawaambieni nitakalolitenda shamba langu la mizabibu; nitaondoa ua wake, nalo litaliwa; nitabomoa ukuta wake, nalo litakanyagwa;


nami nitaliharibu; wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.


Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako.


Nyumba yetu takatifu, nzuri, walimokusifu baba zetu, imeteketea moto; vitu vyetu vyote vyenye kupendeza vimeharibika.


Lakini kama hamtaki kunisikiliza, kuitakasa siku ya sabato, kutokuchukua mzigo katika malango ya Yerusalemu siku ya sabato; basi, nitawasha moto malangoni mwake, nao utaziteketeza nyumba za enzi za Yerusalemu, wala hautazimika.


Maana BWANA wa majeshi Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama hasira yangu, na ghadhabu yangu, ilivyomwagwa juu ya hao wakaao Yerusalemu, ndivyo ghadhabu yangu itakavyomwagwa juu yenu, mtakapoingia Misri; nanyi mtakuwa apizo, na ajabu, na laana, na aibu; wala hamtapaona mahali hapa tena.


Basi, mwambie hivi, BWANA asema hivi, Tazama, niliyoyajenga nitayabomoa, na niliyoyapanda nitayang'oa; na haya yatakuwa katika nchi yote.


Sauti yao wakimbiao na kuokoka, Kutoka katika nchi ya Babeli, Ili kutangaza katika Sayuni kisasi cha BWANA, Mungu wetu, Kisasi cha hekalu lake.


Njia za Sayuni zaomboleza, Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu; Malango yake yote yamekuwa ukiwa, Makuhani wake hupiga kite; Wanawali wake wanahuzunika; Na yeye mwenyewe huona uchungu.


Hasira ya BWANA imewatenga, Yeye hatawaangalia tena; Hawakujali nafsi za wale makuhani, Hawakuwaheshimu wazee wao.


Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA, Alikamatwa katika marima yao; Ambaye kwa habari zake tulisema, Chini ya kivuli chake tutakaa kati ya mataifa.


Wakuu hutundikwa kwa mikono yao; Nyuso za wazee hazipewi heshima.


Kwa maana amekidharau kiapo kwa kulivunja agano; na tazama, ametia mkono wake, na pamoja na hayo ameyatenda mambo hayo yote; hataokoka.


Nami nitaifanya miji yenu iwe maganjo, na mahali penu patakatifu nitapatia ukiwa; wala sitasikia harufu ya manukato yenu yapendezayo.


Nitawakusanya wanaousikitikia mkutano wa ibada, hao waliokuwa wa kwako; ambao mzigo uliokuwa juu yake ulikuwa fedheha kwao.


Kwa sababu hiyo mimi nami nimewafanya ninyi kuwa kitu cha kudharauliwa, na unyonge, mbele ya watu wote, kama vile ninyi msivyozishika njia zangu, bali mmewapendelea watu katika sheria.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo