Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Malaki 3:4 - Swahili Revised Union Version

4 Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za BWANA, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Hivyo, tambiko za watu wa Yuda na wa Yerusalemu zitampendeza Mwenyezi-Mungu kama za watu wa kale; kama katika miaka ya zamani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Hivyo, tambiko za watu wa Yuda na wa Yerusalemu zitampendeza Mwenyezi-Mungu kama za watu wa kale; kama katika miaka ya zamani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Hivyo, tambiko za watu wa Yuda na wa Yerusalemu zitampendeza Mwenyezi-Mungu kama za watu wa kale; kama katika miaka ya zamani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 nazo sadaka za Yuda na Yerusalemu zitakubalika kwa Mwenyezi Mungu, kama katika siku zilizopita, kama katika miaka ya zamani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 nazo sadaka za Yuda na Yerusalemu zitakubalika kwa bwana, kama katika siku zilizopita, kama katika miaka ya zamani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za BWANA, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani.

Tazama sura Nakili

Malaki 3:4
22 Marejeleo ya Msalaba  

hata ikawa, Mungu alipowajalia Walawi waliolichukua sanduku la Agano la BWANA, wakachinja ng'ombe saba, na kondoo dume saba.

Kisha Daudi akamjengea BWANA madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akamlingana BWANA; naye akamwitikia kutoka mbinguni kwa moto juu ya madhabahu hiyo ya sadaka ya kuteketezwa.

Sulemani akaipandia huko madhabahu ya shaba mbele za BWANA, iliyokuwako hemani pa kukutania, akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu yake.

Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.

Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki, Na sadaka za kuteketezwa, na kafara. Ndipo watakapotoa ng'ombe Juu ya madhabahu yako.

Nitawaleta hao nao hadi katika mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.

BWANA asema hivi, Mimi nimerudi Sayuni, nami nitakaa katikati ya Yerusalemu; na Yerusalemu utaitwa, Mji mwaminifu; na mlima wa BWANA wa majeshi utaitwa, mlima mtakatifu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo