Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Malaki 2:16 - Swahili Revised Union Version

16 Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema BWANA wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema: “Ninachukia talaka. Ninachukia mmoja wenu anapomtendea mkewe ukatili huo. Hakikisheni kwamba hakuna hata mmoja wenu anayekosa uaminifu kwa mkewe.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema: “Ninachukia talaka. Ninachukia mmoja wenu anapomtendea mkewe ukatili huo. Hakikisheni kwamba hakuna hata mmoja wenu anayekosa uaminifu kwa mkewe.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema: “Ninachukia talaka. Ninachukia mmoja wenu anapomtendea mkewe ukatili huo. Hakikisheni kwamba hakuna hata mmoja wenu anayekosa uaminifu kwa mkewe.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 “Ninachukia kuachana,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, “pia nachukia mtu anayejivika jeuri kama vazi,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, wala msije mkavunja uaminifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 “Ninachukia kuachana,” asema bwana, Mungu wa Israeli, “pia nachukia mtu anayejivika jeuri kama vazi,” asema bwana Mwenye Nguvu Zote. Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, wala msije mkavunja uaminifu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema BWANA wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.

Tazama sura Nakili

Malaki 2:16
13 Marejeleo ya Msalaba  

Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao, Udhalimu huwavika kama nguo.

Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.

Mwanangu! Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatia kifua cha mgeni?

Maana kitanda kile ni kifupi asiweze mtu kujinyosha juu yake, na nguo ile ya kujifunika ni nyembamba mtu asipate kujizungushia.

BWANA asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo niliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu.

Nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao; kazi zao ni kazi za uovu, na vitendo vya udhalimu vimo mikononi mwao.

Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini.

Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo