Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Luka 24:39 - Swahili Revised Union Version

39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

39 Angalieni mikono na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe. Nipapaseni mkaone, maana mzimu hauna mwili na mifupa kama mnionavyo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

39 Angalieni mikono na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe. Nipapaseni mkaone, maana mzimu hauna mwili na mifupa kama mnionavyo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

39 Angalieni mikono na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe. Nipapaseni mkaone, maana mzimu hauna mwili na mifupa kama mnionavyo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, mwone kuwa ni mimi mwenyewe. Niguseni mwone; kwa maana mzuka huna nyama na mifupa, kama mnavyoniona mimi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, mwone kuwa ni mimi hasa. Niguseni mwone; kwa maana mzuka hauna nyama na mifupa, kama mnionavyo kuwa navyo.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.

Tazama sura Nakili




Luka 24:39
12 Marejeleo ya Msalaba  

Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.


Nao wakaanguka kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote?


Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.


Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu?


Na baada ya kusema hayo aliwaonesha mikono yake na miguu yake.


Naye akiisha kusema hayo, akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana.


Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo.


Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye.


wale aliojidhihirisha kwao kuwa yu hai, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, akiwatokea muda wa siku arubaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.


Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe muwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.


Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawaheshimu; basi si ni afadhali zaidi kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?


Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kuhusu Neno la uzima;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo