Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Luka 17:10 - Swahili Revised Union Version

10 Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Hali kadhalika na nyinyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni: ‘Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa kufanya.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Hali kadhalika na nyinyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni: ‘Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa kufanya.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Hali kadhalika na nyinyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni: ‘Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa kufanya.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Vivyo hivyo nanyi mkishafanya mliyoagizwa, semeni, ‘Sisi tu watumishi tusiostahili; tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa, semeni, ‘Sisi tu watumishi tusiostahili; tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.’ ”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.

Tazama sura Nakili

Luka 17:10
20 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.

Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.

nao wakaingia, wakaimiliki; lakini hawakuitii sauti yako, wala hawakuenda katika sheria yako; hawakutenda neno lolote katika haya uliyowaagiza wayatende; basi, kwa sababu hii umeleta juu yao mabaya haya yote;

Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya.

Je! Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa?

Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena?

Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.

ambaye zamani alikuwa hakufai, bali sasa akufaa sana, wewe na mimi pia;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo