Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 27:1 - Swahili Revised Union Version

1 Nawe fanya madhabahu ya mti wa mshita; urefu wake utakuwa ni dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano; hiyo madhabahu itakuwa mraba; na kwenda juu kwake kutakuwa dhiraa tatu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 “Utatengeneza madhabahu kwa mbao za mjohoro. Madhabahu hiyo itakuwa ya mraba, urefu wake mita mbili na robo, na upana wake mita mbili na robo; kimo chake kitakuwa mita moja na robo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 “Utatengeneza madhabahu kwa mbao za mjohoro. Madhabahu hiyo itakuwa ya mraba, urefu wake mita mbili na robo, na upana wake mita mbili na robo; kimo chake kitakuwa mita moja na robo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 “Utatengeneza madhabahu kwa mbao za mjohoro. Madhabahu hiyo itakuwa ya mraba, urefu wake mita mbili na robo, na upana wake mita mbili na robo; kimo chake kitakuwa mita moja na robo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 “Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake kiwe dhiraa tatu; itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 “Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake kiwe dhiraa tatu; itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano.

Tazama sura Nakili




Kutoka 27:1
20 Marejeleo ya Msalaba  

Siku hiyo Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, Haya! Kwea wewe, ukamwinulie BWANA madhabahu penye kiwanja cha Arauna, Myebusi.


Na ile madhabahu ya shaba iliyokuwako mbele za BWANA, akaileta kutoka mbele ya nyumba, kutoka kati ya madhabahu yake mwenyewe na nyumba ya BWANA, akaiweka upande wa kaskazini wa madhabahu yake.


Lakini Haruni na wanawe ndio waliokuwa wakitoa sadaka juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya madhabahu ya kufukizia uvumba, kwa ajili ya kazi yote ya Patakatifu pa Patakatifu, ili kufanya upatanisho kwa Israeli, kulingana na yote aliyokuwa ameyaamuru Musa, mtumishi wa Mungu.


Tena akafanya madhabahu ya shaba, dhiraa ishirini urefu wake, na dhiraa ishirini upana wake, na dhiraa kumi kwenda juu kwake.


Ndipo akasimama Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zake makuhani, na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na ndugu zake, nao wakaijenga madhabahu ya Mungu wa Israeli, ili kutoa sadaka za kuteketezwa juu yake, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, mtu wa Mungu.


Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yahweh-nisi;


Basi Musa akayaandika maneno yote ya BWANA, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya makabila kumi na mawili ya Israeli,


na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, na birika na kitako chake;


na hiyo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, pamoja na wavu wake wa shaba, miti yake, vyombo vyake vyote hilo birika na kitako chake;


na madhabahu ya shaba, na wavu wake wa shaba, na miti yake, na vyombo vyake vyote, na birika na kitako chake;


Kisha utaitia mafuta madhabahu ya kuteketeza sadaka, na vyombo vyake vyote; na kuiweka takatifu madhabahu; na hiyo madhabahu itakuwa takatifu sana.


Akaiweka madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mlangoni pa maskani ya kukutania, akatoa sadaka ya kuteketezwa juu yake, na sadaka ya unga; kama BWANA alivyomwamuru Musa.


Kisha utaweka madhabahu ya kuteketeza sadaka mbele ya mlango wa maskani ya hema ya kukutania.


Na vitu watakavyovitunza ni hilo sanduku, na meza, na kinara cha taa, na madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu wavitumiavyo katika huduma yao, na pazia, na utumishi wake wote.


Nao watayaondoa hayo majivu madhabahuni; na kutandika nguo ya rangi ya zambarau juu yake;


nao wataweka vyombo vyake vyote juu yake ambavyo wavitumia katika madhabahu, vyetezo, na nyuma, na miiko, na mabakuli, vyombo vyote vya hiyo madhabahu; nao watatandika juu yake ngozi za pomboo, na kutia miti yake mahali pake.


Tuna madhabahu ambayo wale waihudumiayo ile hema hawana ruhusa kula vitu vyake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo