Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 11:1 - Swahili Revised Union Version

1 BWANA akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Bado kuna pigo moja nitakalomletea Farao na nchi ya Misri. Baadaye atawaacheni mwondoke hapa. Tena atakapowaacheni mwondoke, yeye mwenyewe atawafukuza mwondoke kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Bado kuna pigo moja nitakalomletea Farao na nchi ya Misri. Baadaye atawaacheni mwondoke hapa. Tena atakapowaacheni mwondoke, yeye mwenyewe atawafukuza mwondoke kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Bado kuna pigo moja nitakalomletea Farao na nchi ya Misri. Baadaye atawaacheni mwondoke hapa. Tena atakapowaacheni mwondoke, yeye mwenyewe atawafukuza mwondoke kabisa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Basi Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Musa, “Nitaleta pigo moja zaidi kwa Farao na katika nchi ya Misri. Baada ya hilo, atawaacha mwondoke hapa na atakapofanya hivyo, atawafukuza mtoke kabisa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Basi bwana alikuwa amemwambia Musa, “Nitaleta pigo moja zaidi kwa Farao na katika nchi ya Misri. Baada ya hilo, atawaacha mwondoke hapa na atakapofanya hivyo, atawafukuza mtoke kabisa.

Tazama sura Nakili




Kutoka 11:1
11 Marejeleo ya Msalaba  

Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali nyingi.


Wewe unafanya upya ushahidi wako juu yangu, Na kuongeza kisirani chako juu yangu; Ukileta jeshi baada ya jeshi juu yangu.


Hata ikawa, usiku wa manane BWANA akawaua wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hadi mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama.


Nami nitaunyosha mkono wangu, na kuipiga Misri kwa ajabu zangu zote, nitakazofanya kati yake, kisha baadaye atawapa ruhusa kwenda.


BWANA akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake.


Kwani wakati huu nitaleta mapigo yangu yote juu ya moyo wako, na juu ya watumishi wako, na juu ya watu wako; ili upate kujua ya kuwa hapana mmoja mfano wa mimi ulimwenguni kote.


Nanyi ikiwa mnaenda kinyume changu, wala hamtaki kunisikiza; nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, kama dhambi zenu zilivyo.


Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa kutoka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, ishara, maajabu, vita, mkono hodari, mkono ulionyoshwa, na vitisho vikuu, kama vile BWANA, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu?


Wanadamu wakaunguzwa na joto kali, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.


Ndipo wakauliza, Na hayo matoleo ya kosa tutakayompelekea, yatakuwa ya namna gani? Na yawe majipu ya dhahabu matano, na panya wa dhahabu watano, sawasawa na idadi ya wakuu wa Wafilisti; kwa kuwa tauni moja ilikuwa juu yenu nyote, na juu ya wakuu wenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo