Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 9:20 - Swahili Revised Union Version

20 Hupokonya upande wa mkono wa kulia, nao huona njaa! Hula upande wa mkono wa kushoto, wala hawashibi! Watakula kila mtu nyama ya mkono wake mwenyewe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 wananyanganya upande mmoja na hawatosheki; wanakula upande mwingine lakini hawashibi. Kila mmoja anamshambulia mwenzake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 wananyanganya upande mmoja na hawatosheki; wanakula upande mwingine lakini hawashibi. Kila mmoja anamshambulia mwenzake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 wananyang'anya upande mmoja na hawatosheki; wanakula upande mwingine lakini hawashibi. Kila mmoja anamshambulia mwenzake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Upande wa kuume watakuwa wakitafuna, lakini bado wataona njaa; upande wa kushoto watakuwa wakila, lakini hawatashiba. Kila mmoja atajilisha kwa nyama ya uzao wake mwenyewe:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Upande wa kuume watakuwa wakitafuna, lakini bado wataona njaa; upande wa kushoto watakuwa wakila, lakini hawatashiba. Kila mmoja atajilisha kwa nyama ya mtoto wake mwenyewe:

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

20 Hupokonya upande wa mkono wa kulia, nao huona njaa! Hula upande wa mkono wa kushoto, wala hawashibi! Watakula kila mtu nyama ya mkono wake mwenyewe.

Tazama sura Nakili




Isaya 9:20
16 Marejeleo ya Msalaba  

Mpumbavu huikunja mikono yake, Naye hula chakula chake mwenyewe;


Watainama chini ya wafungwa tu, wataanguka chini yao waliouawa. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.


Nao walio maskini kabisa watakula, Na wahitaji watajilaza salama; Nami nitatia shina lako kwa njaa, Na mabaki yako watauawa.


Kwa maana, tazama, Bwana, BWANA wa majeshi, awaondolea Yerusalemu na Yuda egemeo na tegemeo; tegemeo lote la chakula na tegemeo lote la maji;


Na hao wanaokuonea nitawalisha nyama yao wenyewe, nao watalewa kwa kuinywa damu yao wenyewe, kama kwa mvinyo mpya; na watu wote watajua ya kuwa mimi, BWANA, ni mwokozi wako, na Mkombozi wako ni Mwenye enzi wa Yakobo.


Kwa sababu hiyo hasira ya BWANA imewaka juu ya watu wake, naye amenyosha mkono wake juu yao; akawapiga, navyo vilima vilitetemeka, na mizoga yao ilikuwa kama takataka katika njia kuu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.


Mambo haya mawili yamekupata; Ni nani awezaye kukusikitikia? Ukiwa na uharibifu, na njaa na upanga; Niwezeje kukutuliza?


Nao watapita katikati yake, wamedhikika sana na kuwa na njaa; na itakuwa watakapoona njaa, watalalamika na kuapa kwa mfalme wao, na kwa Mungu wao, na kuelekeza nyuso zao juu;


nao wataiangalia nchi, na, tazama, shida na giza; hapatakuwa changamko kwa sababu ya dhiki; nao watafukuzwa na kuingia katika giza kubwa.


Nitawagonganisha, mtu na mwenzake, naam, baba za watu na watoto wao pamoja, asema BWANA; sitahurumia, wala sitaachilia, wala sitarehemu, hata nisiwaangamize.


Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawatesa.


Mikono ya wanawake wenye huruma Imewatokosa watoto wao wenyewe; Walikuwa ndio chakula chao Katika uharibifu wa binti ya watu wangu.


Utakula, lakini hutashiba; ndani yenu njaa itazidi kuwauma; nawe utahama, lakini hutachukua kitu salama; na hicho utakachochukua nitakitoa kwa upanga.


Ndipo nikasema, Sitawalisheni; afaye na afe; atakayekatiliwa mbali na akatiliwe mbali; nao waliosalia, kila mmoja na ale nyama ya mwili wa mwenziwe.


Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo