Isaya 9:18 - Swahili Revised Union Version18 Kwa maana uovu huteketeza kama moto; huila mibigili na miiba, naam, huwaka katika vichaka vya mwitu, nao hupaa juu katika mawingu mazito ya moshi. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema18 Uovu huwaka kama moto uteketezao mbigili na miiba; huwaka kama moto msituni, na kutoa moshi mzito upandao angani juu. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND18 Uovu huwaka kama moto uteketezao mbigili na miiba; huwaka kama moto msituni, na kutoa moshi mzito upandao angani juu. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza18 Uovu huwaka kama moto uteketezao mbigili na miiba; huwaka kama moto msituni, na kutoa moshi mzito upandao angani juu. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu18 Hakika uovu huwaka kama moto; huteketeza michongoma na miiba, huwasha moto vichaka vya msituni, hujiviringisha kuelekea juu kama nguzo ya moshi. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu18 Hakika uovu huwaka kama moto; huteketeza michongoma na miiba, huwasha moto vichaka vya msituni, hujiviringisha kuelekea juu kama nguzo ya moshi. Tazama suraBIBLIA KISWAHILI18 Kwa maana uovu huteketeza kama moto; huila mibigili na miiba, naam, huwaka katika vichaka vya mwitu, nao hupaa juu katika mawingu mazito ya moshi. Tazama sura |
Kwa hiyo kama vile muali wa moto uteketezavyo mabua makavu, na kama manyasi makavu yaangukavyo katika muali wa moto; kadhalika shina lao litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi, na kulidharau neno lake aliye Mtakatifu wa Israeli.
lakini jeshi lililotoka kaskazini nitaliondolea mbali nanyi, nami nitalifukuza mpaka nchi ya ukame na ukiwa; sehemu yake iliyo mbele itaingia katika bahari ya mashariki, na sehemu yake iliyo nyuma itaingia katika bahari ya magharibi; na uvundo wake utapanda juu, na harufu yake mbaya itapanda juu, kwa sababu ametenda mambo makubwa.