Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 9:14 - Swahili Revised Union Version

14 Kwa sababu hiyo BWANA atakata katika Israeli kichwa na mkia, kuti na nyasi, katika siku moja.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Basi kwa muda wa siku moja tu, Mwenyezi-Mungu atakata katika Israeli vichwa na mikia, tawi la mtende na nyasi:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Basi kwa muda wa siku moja tu, Mwenyezi-Mungu atakata katika Israeli vichwa na mikia, tawi la mtende na nyasi:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Basi kwa muda wa siku moja tu, Mwenyezi-Mungu atakata katika Israeli vichwa na mikia, tawi la mtende na nyasi:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu atakatilia mbali kutoka Israeli kichwa na mkia, tawi la mtende na tete katika siku moja.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kwa hiyo bwana atakatilia mbali kutoka Israeli kichwa na mkia, tawi la mtende na tete katika siku moja.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Kwa sababu hiyo BWANA atakata katika Israeli kichwa na mkia, kuti na nyasi, katika siku moja.

Tazama sura Nakili




Isaya 9:14
28 Marejeleo ya Msalaba  

Na mwanga wa Israeli utakuwa ni moto, na Mtakatifu wake atakuwa muali wa moto; nao utateketeza na kula mbigili zake na miiba yake kwa siku moja.


Wala haitakuwako kazi yoyote katika Misri iwezayo kufanywa, ya kichwa au ya mkia, ya tawi au ya nyasi.


basi, uovu huu utakuwa kwenu kama mahali palipobomoka, kuanguka patokezapo katika ukuta mrefu, ambapo kuvunjika kwake huja ghafla kwa mara moja.


Basi, kwa hiyo, BWANA asema hivi, Tazama, nitaweka makwazo mbele ya watu hawa, na baba na wana wao watajikwaa pamoja; jirani ya mtu na rafiki yake watapotea.


Je! Waliona aibu, walipokuwa wametenda machukizo? La! Hawakuona aibu kabisa, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi wataanguka miongoni mwao waangukao; wakati wa kujiliwa kwao wataangushwa chini, asema BWANA.


Hasira ya BWANA imewatenga, Yeye hatawaangalia tena; Hawakujali nafsi za wale makuhani, Hawakuwaheshimu wazee wao.


BWANA akamwambia, Mwite jina lake Yezreeli; kwa maana bado kitambo kidogo, nitaipatiliza nyumba ya Yehu damu ya Yezreeli, na kuukomesha ufalme wa nyumba ya Israeli.


Akachukua mimba tena, akazaa mtoto wa kike, BWANA akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama; kwa maana sitairehemu nyumba ya Israeli tena, nisije nikawasamehe kwa njia yoyote.


BWANA akasema, Mwite jina lake Lo-ami; kwa maana ninyi si watu wangu, wala mimi sitakuwa Mungu wenu.


Hivyo ndivyo Betheli atakavyowatenda ninyi, kwa sababu ya ubaya wenu mwingi; wakati wa mapambazuko mfalme wa Israeli atakatiliwa mbali kabisa.


Kwa sababu hiyo watakuwa kama wingu la asubuhi, na kama umande utowekao upesi, kama makapi yaliyopeperushwa na tufani sakafuni, na kama moshi utokao katika bomba.


Na wewe utajikwaa wakati wa mchana, na nabii naye atajikwaa pamoja nawe wakati wa usiku; nami nitamwangamiza mama yako.


Israeli amemezwa; sasa wamo miongoni mwa mataifa kama chombo kisichopendeza.


Haya ndiyo asemayo BWANA; Kama vile mchungaji apokonyavyo kinywani mwa simba miguu miwili, au kipande cha sikio; ndivyo watakavyopokonywa wana wa Israeli, wakaao Samaria katika pembe ya kochi, na juu ya mito ya hariri ya kitanda.


Kwa maana, angalia, BWANA atoa amri, na jumba kuu litabomolewa vipande vipande, na nyumba ndogo kuwa vigae.


kwa hiyo, BWANA asema hivi, Mke wako atakuwa kahaba mjini, na wana wako na binti zako wataanguka kwa upanga, na shamba lako litagawanywa kwa kamba; na wewe mwenyewe utakufa katika nchi iliyo najisi; na bila shaka Israeli atapelekwa uhamishoni mbali na nchi yake.


wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.


kwa kuwa katika saa moja utajiri mwingi namna hii umekuwa ukiwa. Na kila nahodha na kila aendaye mahali popote kwa matanga, na mabaharia, nao wote watendao kazi baharini, wakasimama mbali;


Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo