Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 9:11 - Swahili Revised Union Version

11 Kwa sababu hiyo BWANA atawainua adui wa Resini juu yake, naye atawachochea adui zake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Basi, Mwenyezi-Mungu atawaletea wapinzani na kuwachochea maadui zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Basi, Mwenyezi-Mungu atawaletea wapinzani na kuwachochea maadui zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Basi, Mwenyezi-Mungu atawaletea wapinzani na kuwachochea maadui zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Lakini Mwenyezi Mungu amemtia nguvu adui wa Resini dhidi yao na kuchochea watesi wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Lakini bwana amemtia nguvu adui wa Resini dhidi yao na kuchochea watesi wao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Kwa sababu hiyo BWANA atawainua adui wa Resini juu yake, naye atawachochea adui zake;

Tazama sura Nakili




Isaya 9:11
10 Marejeleo ya Msalaba  

Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.


Na huyo mfalme wa Ashuru akamsikia; mfalme wa Ashuru akapanda juu ya Dameski, akautwaa, akawahamisha watu wake mateka mpaka Kiri, akamwua Resini.


Watainama chini ya wafungwa tu, wataanguka chini yao waliouawa. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.


Ole wa taji la kiburi la walevi wa Efraimu, na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, la hao walioshindwa na divai!


Kwa sababu hiyo hasira ya BWANA imewaka juu ya watu wake, naye amenyosha mkono wake juu yao; akawapiga, navyo vilima vilitetemeka, na mizoga yao ilikuwa kama takataka katika njia kuu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.


Hata ikawa katika siku za Ahazi, mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, mfalme wa Yuda, Resini, mfalme wa Shamu, na Peka, mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, wakapanda wakaenda Yerusalemu ili kupigana nao, lakini hawakuweza kuushinda.


Kwa maana kichwa cha Shamu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini; na katika muda wa miaka sitini na mitano Efraimu atavunjika vipande vipande, asiwe kabila la watu tena;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo