Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 60:5 - Swahili Revised Union Version

5 Ndipo utakapoona na kutiwa nuru, Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia, Utajiri wa mataifa utakuwasilia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Utaona na uso wako utangara, moyo wako utasisimka na kushangilia. Maana utajiri wa bahari utakutiririkia, mali za mataifa zitaletwa kwako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Utaona na uso wako utangara, moyo wako utasisimka na kushangilia. Maana utajiri wa bahari utakutiririkia, mali za mataifa zitaletwa kwako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Utaona na uso wako utang'ara, moyo wako utasisimka na kushangilia. Maana utajiri wa bahari utakutiririkia, mali za mataifa zitaletwa kwako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Ndipo utatazama na kutiwa nuru, moyo wako utasisimka na kujaa furaha, mali iliyo baharini italetwa kwako, utajiri wa mataifa utakujilia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Ndipo utatazama na kutiwa nuru, moyo wako utasisimka na kujaa furaha, mali zilizo baharini zitaletwa kwako, utajiri wa mataifa utakujilia.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Ndipo utakapoona na kutiwa nuru, Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia, Utajiri wa mataifa utakuwasilia.

Tazama sura Nakili




Isaya 60:5
25 Marejeleo ya Msalaba  

Nitakwenda mbio katika njia ya maagizo yako, Utakaponipanulia ufahamu wangu.


Mwelekezeeni macho, mpate kufurahi, Na nyuso zenu hazitaaibishwa kamwe.


Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.


Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako.


Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Huku wakiwaongoza wafalme wao.


Bali ninyi mtaitwa makuhani wa BWANA; watu watawaiteni wahudumu wa Mungu wetu; mtakula utajiri wa mataifa, na kujisifia utukufu wao.


Maana BWANA asema hivi, Tazama, nitamwelekezea amani kama mto, na utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa; na juu ya magoti mtabembelezwa.


Na mji huu utakuwa kwangu jina la furaha, na sifa na utukufu, mbele ya mataifa yote ya dunia, watakaosikia habari ya mema yote niwatendeayo, nao wataogopa na kutetemeka, kwa sababu ya mema yote na amani nitakaoupatia mji huo.


baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta BWANA, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea BWANA na wema wake kwa kicho siku za mwisho.


Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.


Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.


Basi ikiwa Mwenyezi Mungu amewapa wao karama ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu?


Baada ya miaka mingi nilifika niwaletee watu wa taifa langu sadaka na matoleo.


Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.


maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kutoa mchango kwa ajili ya watakatifu walio maskini huko Yerusalemu.


wala hatujisifu zaidi ya kadiri yetu, yaani, katika taabu za watu wengine; bali tukiwa na tumaini ya kwamba, imani yenu ikuapo, tutakuzwa kwenu kwa kadiri ya kipimo chetu, na kupata ziada;


Watayaita mataifa waje mlimani; Wakasongeze huko sadaka za haki; Kwa kuwa watanyonya wingi wa bahari, Na akiba zilizofichamana za mchangani.


Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.


Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.


Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia BWANA, Pembe yangu imetukuka katika BWANA, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo