Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 60:22 - Swahili Revised Union Version

22 Aliye mdogo zaidi atakuwa elfu, Na mnyonge atakuwa taifa hodari; Mimi, BWANA, nitayahimiza hayo wakati wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Aliye mdogo kati yenu atakuwa ukoo, aliye mdogo kuliko wote atakuwa taifa kubwa. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu; wakati ufikapo nitayatekeleza hayo haraka.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Aliye mdogo kati yenu atakuwa ukoo, aliye mdogo kuliko wote atakuwa taifa kubwa. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu; wakati ufikapo nitayatekeleza hayo haraka.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Aliye mdogo kati yenu atakuwa ukoo, aliye mdogo kuliko wote atakuwa taifa kubwa. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu; wakati ufikapo nitayatekeleza hayo haraka.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Aliye mdogo kwenu atakuwa elfu, mdogo kuliko wote atakuwa taifa lenye nguvu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu; katika wakati wake nitayatimiza haya upesi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Aliye mdogo kwenu atakuwa elfu, mdogo kuliko wote atakuwa taifa lenye nguvu. Mimi ndimi bwana; katika wakati wake nitayatimiza haya upesi.”

Tazama sura Nakili




Isaya 60:22
15 Marejeleo ya Msalaba  

Maana watu wako, Ee Israeli, wajapokuwa wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki tu watakaorudi; kuangamiza kumekusudiwa, kunakofurika kwa haki.


Wasema, Na afanye haraka, aihimize kazi yake, tupate kuiona; na likaribie shauri lake aliye Mtakatifu wa Israeli, tupate kuliona.


Mwangalieni Abrahamu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa; kwa maana alipokuwa mmoja tu nilimwita, nikambariki, nikamfanya kuwa wengi.


Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara? Maana Sayuni, mara alipopata uchungu, Alizaa watoto wake.


Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa joto; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.


Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.


Nami nitamfanya yeye aliyechechemea kuwa mabaki, na yeye aliyetupwa mbali kuwa taifa lenye nguvu, na BWANA atawamiliki katika mlima Sayuni tangu sasa na hata milele.


Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.


Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?


Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapatao elfu tatu.


walioamini wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake;


Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi.


Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.


Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo