Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 6:3 - Swahili Revised Union Version

3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Waliitana kila mmoja na mwenzake hivi: “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Dunia yote imejaa utukufu wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Waliitana kila mmoja na mwenzake hivi: “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Dunia yote imejaa utukufu wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Waliitana kila mmoja na mwenzake hivi: “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Dunia yote imejaa utukufu wake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni; dunia yote imejaa utukufu wake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni bwana Mwenye Nguvu Zote; dunia yote imejaa utukufu wake.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.

Tazama sura Nakili




Isaya 6:3
25 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaimbiana, wakimhimidi BWANA, na kumshukuru, wakasema, Kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele. Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi BWANA, kwa sababu msingi wa nyumba ya BWANA umekwisha kuwekwa.


Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.


Imbeni utukufu wa jina lake, Tukuzeni sifa zake.


Jina lake tukufu na lihimidiwe milele; Dunia yote na ijae utukufu wake. Amina na Amina.


Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mjilipiza kisasi.


Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako, Na utukufu wako kwa watoto wao.


Mbingu zimetangaza haki yake, Na watu wote wameuona utukufu wake.


Na walisifu jina lake kuu litishalo; Ndiye mtakatifu.


Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana BWANA, Mungu wetu, ni mtakatifu.


Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?


Toka pande za mwisho wa dunia tumesikia nyimbo, Atukuzwe mwenye haki. Ndipo niliposema, Kukonda kwangu! Kukonda kwangu! Ole wangu! Watenda hila wametenda hila, naam, watendao hila wametenda hila sana.


Na utukufu wa BWANA utafunuliwa, Na watu wote watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha BWANA kimenena haya.


Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.


na tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulitokea kwa njia ya mashariki; na sauti yake ilikuwa kama mshindo wa maji mengi, nayo nchi iling'aa kwa utukufu wake.


Kisha akanileta, kwa njia ya lango la upande wa kaskazini, mbele ya nyumba; nikaangalia, na tazama, huo utukufu wa BWANA uliijaza nyumba ya BWANA; nikaanguka kifudifudi.


Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa BWANA, kama maji yaifunikavyo bahari.


Naye BWANA atakuwa Mfalme wa nchi yote; siku hiyo BWANA atakuwa mmoja, na jina lake moja.


lakini hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na utukufu wa BWANA;


macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo