Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 49:24 - Swahili Revised Union Version

24 Je! Aliye hodari aweza kunyang'anywa mateka wake, au mateka wa mtu katili kuokoka?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Watu wa Yerusalemu walalamika: “Je, shujaa aweza kunyanganywa nyara zake? Au mateka wa mtu katili waweza kuokolewa?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Watu wa Yerusalemu walalamika: “Je, shujaa aweza kunyanganywa nyara zake? Au mateka wa mtu katili waweza kuokolewa?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Watu wa Yerusalemu walalamika: “Je, shujaa aweza kunyang'anywa nyara zake? Au mateka wa mtu katili waweza kuokolewa?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Je, nyara zaweza kuchukuliwa kutoka kwa mashujaa wa vita, au mateka kuokolewa kutoka kwa watu wakali?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Je, nyara zaweza kuchukuliwa kutoka kwa mashujaa wa vita, au mateka kuokolewa kutoka kwa watu wakali?

Tazama sura Nakili




Isaya 49:24
17 Marejeleo ya Msalaba  

Na baada ya hayo yote yaliyotupata kwa sababu ya matendo yetu mabaya, na kwa sababu ya hatia yetu iliyo kuu, ikiwa wewe Mungu wetu hukutuadhibu kama tulivyostahili kwa maovu yetu, maana umetupa mabaki;


Maana sisi tu watumwa; lakini Mungu wetu hakutuacha katika utumwa wetu, bali ametufikishia rehema zake, mbele ya wafalme wa Uajemi, ili kutupa maisha mapya, kuisimamisha nyumba ya Mungu wetu, na kuitengeneza palipobomoka, na atulinde katika Yuda na Yerusalemu.


Lakini wewe u mwenye haki, katika hayo yote yaliyotupata; maana wewe umetenda yaliyo kweli, lakini sisi tumetenda yaliyo maovu;


Nayo yawapatia faida nyingi wafalme uliowaweka kututawala kwa sababu ya dhambi zetu; tena wana mamlaka juu ya miili yetu, na juu ya wanyama wetu, kadiri wapendavyo, nasi tuko katika dhiki kuu.


Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.


Ngurumo yao itakuwa kama ya simba; Watanguruma kama wanasimba; Naam, watanguruma na kukamata mateka, Na kuyachukua na kwenda zao salama, Wala hakuna mtu atakayeokoa.


Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawana nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.


Kisha akaniambia, Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli; tazama, wao husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini yetu yametupotea; tumekatiliwa mbali kabisa.


Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe.


Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawaangamiza wanasimba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.


Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake.


Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo