Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 45:6 - Swahili Revised Union Version

6 ili wapate kujua toka maawio ya jua, na toka magharibi, ya kuwa hapana mwingine zaidi ya mimi; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 ili watu wote, toka mashariki hadi magharibi, wajue kwamba hakuna Mungu mwingine ila mimi; mimi ni Mwenyezi-Mungu na hakuna mwingine.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 ili watu wote, toka mashariki hadi magharibi, wajue kwamba hakuna Mungu mwingine ila mimi; mimi ni Mwenyezi-Mungu na hakuna mwingine.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 ili watu wote, toka mashariki hadi magharibi, wajue kwamba hakuna Mungu mwingine ila mimi; mimi ni Mwenyezi-Mungu na hakuna mwingine.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 ili kutoka mawio ya jua hadi machweo yake, watu wapate kujua kwamba hakuna Mungu mwingine ila Mimi. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu wala hakuna mwingine.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 ili kutoka mawio ya jua mpaka machweo yake, watu wapate kujua kwamba hakuna Mungu mwingine ila Mimi. Mimi ndimi bwana wala hakuna mwingine.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 ili wapate kujua toka mawio ya jua, na toka magharibi, ya kuwa hapana mwingine zaidi ya mimi; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.

Tazama sura Nakili




Isaya 45:6
16 Marejeleo ya Msalaba  

Tulieni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.


Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye Juu, juu ya nchi yote.


Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua BWANA, kama vile maji yanavyoifunika bahari.


Basi sasa, BWANA, Mungu wetu, utuokoe kutoka kwa mkono wake, falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe BWANA, wewe peke yako.


Ninyi ni mashahidi wangu, asema BWANA, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine.


BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.


Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakuimarisha ijapokuwa hukunijua;


Sasa, basi, sikia haya, wewe upendaye anasa, ukaaye na kujiona salama, wewe usemaye moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi; sitaketi kama mjane, wala sitajua kufiwa na watoto;


Na hao wanaokuonea nitawalisha nyama yao wenyewe, nao watalewa kwa kuinywa damu yao wenyewe, kama kwa mvinyo mpya; na watu wote watajua ya kuwa mimi, BWANA, ni mwokozi wako, na Mkombozi wako ni Mwenye enzi wa Yakobo.


Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA.


Nami nitajitukuza, na kujitakasa, na kujidhihirisha, mbele ya macho ya mataifa mengi; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Nami nitauweka utukufu wangu kati ya mataifa, na mataifa wote wataiona hukumu yangu niliyoitekeleza, na mkono wangu niliouweka juu yao.


Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe.


Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo