Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 43:16 - Swahili Revised Union Version

16 BWANA asema hivi, yeye afanyaye njia katika bahari; na mahali pa kupita katika maji yenye nguvu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wakati mmoja nilifanya barabara baharini nikaweka njia kati ya mawimbi makubwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wakati mmoja nilifanya barabara baharini nikaweka njia kati ya mawimbi makubwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wakati mmoja nilifanya barabara baharini nikaweka njia kati ya mawimbi makubwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, yeye aliyefanya njia baharini, mahali pa kupita kwenye maji mengi,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Hili ndilo asemalo bwana, yeye aliyefanya njia baharini, mahali pa kupita kwenye maji mengi,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 BWANA asema hivi, yeye afanyaye njia katika bahari; na mahali pa kupita katika maji yenye nguvu;

Tazama sura Nakili




Isaya 43:16
21 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe uliipasua bahari mbele yao, hata wakapita katikati ya bahari katika nchi kavu; na wale waliokuwa wakiwafuatia ukawatupa vilindini, kama jiwe katika maji makuu.


Akaikemea Bahari ya Shamu ikakauka, Akawaongoza vilindini kana kwamba ni nchi kavu.


Njia yako ilikuwa katika bahari. Na mapito yako yalikuwa katika maji makuu; Hatua zako hazikujulikana.


Uliwaongoza watu wako kama kundi, Kwa mkono wa Musa na Haruni.


Aliipasua bahari akawavusha; Aliyafanya maji yasimame kama ukuta.


Nawe inua fimbo yako, ukanyoshe mkono wako juu ya bahari, na kuigawanya; nao wana wa Israeli watapita kati ya bahari katika nchi kavu.


Lakini wana wa Israeli wakaenda katika nchi kavu katikati ya bahari; na hayo maji yalikuwa ni kuta upande wao wa kulia, na upande wao wa kushoto.


Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.


niviambiaye vilindi, Kauka, nami nitaikausha mito yako;


Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu.


Si wewe uliyemkatakata Rahabu? Uliyemchoma yule joka? Si wewe uliyeikausha bahari, Na maji ya vilindi vikuu; Uliyevifanya vilindi kuwa njia, Ili wapite watu waliokombolewa?


Maana mimi ni BWANA, Mungu wako, niichafuaye bahari, mawimbi yake yakavuma.


BWANA asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku, aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; BWANA wa majeshi, ndilo jina lake;


Na huyo wa sita akalimimina bakuli lake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo