Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 41:21 - Swahili Revised Union Version

21 Haya, leteni maneno yenu, asema BWANA; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Mwenyezi-Mungu, Mfalme wa Yakobo, asema: “Enyi miungu ya mataifa, njoni mtoe hoja zenu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Mwenyezi-Mungu, Mfalme wa Yakobo, asema: “Enyi miungu ya mataifa, njoni mtoe hoja zenu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Mwenyezi-Mungu, Mfalme wa Yakobo, asema: “Enyi miungu ya mataifa, njoni mtoe hoja zenu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Mwenyezi Mungu asema, “Leta shauri lako. Toa hoja yako,” asema Mfalme wa Yakobo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 bwana asema, “Leta shauri lako. Toa hoja yako,” asema Mfalme wa Yakobo.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

21 Haya, leteni maneno yenu, asema BWANA; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo.

Tazama sura Nakili




Isaya 41:21
12 Marejeleo ya Msalaba  

Ningemwambia hesabu ya hatua zangu Ningemkaribia kama vile mkuu.


Basi jifunge viuno kama mwanamume, Maana nitakuuliza neno, nawe niambie.


Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama damu, zitakuwa kama sufu.


Kwa maana BWANA ndiye mwamuzi wetu; BWANA ndiye mfanya sheria wetu; BWANA ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.


Nyamazeni mbele zangu, enyi visiwa, na mataifa wajipatie nguvu mpya; na waje karibu wakanene; na tukaribiane pamoja kwa hukumu.


Mimi ni BWANA, Mtakatifu wenu, Muumba wa Israeli, mfalme wenu.


Na wakusanyike mataifa yote, kabila zote wakutanike; ni nani miongoni mwao awezaye kuhubiri neno hili, na kutuonesha mambo ya zamani? Na walete mashahidi wao, wapate kuhesabiwa kuwa na haki; au na wasikie, wakaseme, Ni kweli.


BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.


nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo