Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 3:17 - Swahili Revised Union Version

17 Basi, kwa hiyo, Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na BWANA ataifunua aibu yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nitawaadhibu; nitawanyoa nywele hao wanawake wa Siyoni, na kuwavua nguo za kufunika uchi wao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nitawaadhibu; nitawanyoa nywele hao wanawake wa Siyoni, na kuwavua nguo za kufunika uchi wao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nitawaadhibu; nitawanyoa nywele hao wanawake wa Siyoni, na kuwavua nguo za kufunika uchi wao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Kwa hiyo Bwana ataleta majipu kwenye vichwa vya wanawake wa Sayuni; Mwenyezi Mungu atazifanya ngozi za vichwa vyao kuwa vipara.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kwa hiyo Bwana ataleta majipu kwenye vichwa vya wanawake wa Sayuni; bwana atazifanya ngozi za vichwa vyao kuwa vipara.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

17 Basi, kwa hiyo, Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na BWANA ataifunua aibu yao.

Tazama sura Nakili




Isaya 3:17
15 Marejeleo ya Msalaba  

Tokeni, enyi binti za Sayuni, Mtazameni Mfalme Sulemani, Amevaa taji alilovikwa na mamaye, Siku ya posa yake, Siku ya furaha ya moyo wake.


vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawachukua uchi, wafungwa wa Misri, na watu wa Kushi waliohamishwa, watoto kwa wazee, bila viatu, matako yao wazi, Misri iaibishwe.


BWANA akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;


Siku hiyo BWANA atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;


Nawe ukisema moyoni mwako, Mbona mambo haya yamenipata mimi? Ni kwa sababu ya wingi wa uovu wako, marinda yako yamefunuliwa, na visigino vya miguu yako vimeumia.


au aliye na kibyongo, au aliyedumaa, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu;


Piteni; njia yenu, wakazi wa Shafiri, mkiwa uchi na wenye aibu; Wakazi wa Saanani msitokeze nje; Beth-eseli unalia na ataondoa msaada wake kwenu;


Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi; nami nitayainua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako.


BWANA atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.


Akaenda huyo wa kwanza, akalimimina bakuli lake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo