Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 26:9 - Swahili Revised Union Version

9 Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema; Maana hukumu zako zikiwapo duniani, Watu wakaao duniani hujifunza haki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Moyo wangu wakutamani usiku kucha, nafsi yangu yakutafuta kwa moyo. Utakapoihukumu dunia, watu wote ulimwenguni watajifunza haki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Moyo wangu wakutamani usiku kucha, nafsi yangu yakutafuta kwa moyo. Utakapoihukumu dunia, watu wote ulimwenguni watajifunza haki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Moyo wangu wakutamani usiku kucha, nafsi yangu yakutafuta kwa moyo. Utakapoihukumu dunia, watu wote ulimwenguni watajifunza haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Nafsi yangu yakutamani wakati wa usiku, wakati wa asubuhi roho yangu yakuonea shauku. Hukumu zako zinapokuja juu ya dunia, watu wa ulimwengu hujifunza haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Nafsi yangu yakutamani wakati wa usiku, wakati wa asubuhi roho yangu yakuonea shauku. Wakati hukumu zako zinapokuja juu ya dunia, watu wa ulimwengu hujifunza haki.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema; Maana hukumu zako zikiwapo duniani, Watu wakaao duniani hujifunza haki.

Tazama sura Nakili




Isaya 26:9
28 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu; Duniani kote kuna hukumu zake.


Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu; Hukumu zake ziko duniani kote.


Wakati wa usiku nimelikumbuka jina lako, Ee BWANA, nikaitii sheria yako.


Usiku wa manane nitaamka nikushukuru, Kwa sababu ya hukumu zako za haki.


Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi.


Na mwanadamu atasema, Hakika iko thawabu yake mwenye haki. Hakika yuko Mungu Anayehukumu katika dunia.


Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.


Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.


Na watu wote wataogopa, Wataitangaza kazi ya Mungu, Na kuyafahamu matendo yake.


Alipowaua ndipo walipokuwa wakimtafuta; Wakarudi wakamtaka Mungu kwa bidii.


Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye Juu, juu ya nchi yote.


Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.


Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena.


Ni nani miongoni mwenu amchaye BWANA, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la BWANA, na kumtegemea Mungu wake.


Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yuko karibu;


Inuka, ulalamike usiku, Mwanzo wa mikesha yake; Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana; Umwinulie mikono yako; Kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa, Mwanzo wa kila njia kuu.


BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo.


Nayo itakuwa tukano na aibu, na mafundisho na ajabu, kwa mataifa wakuzungukao, hapo nitakapotekeleza hukumu ndani yako, kwa hasira, na kwa ghadhabu, na kwa adhabu kali; mimi, BWANA, nimeyanena hayo;


Nitakwenda zangu niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.


Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.


Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.


Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu.


Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliobakia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo