Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Isaya 22:25 - Swahili Revised Union Version

25 Katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, ule msumari uliokazwa katika mahali palipo imara utalegea; nao utakatwa na kuanguka chini, na ule mzigo uliokuwa juu yake utakatiliwa mbali; maana BWANA amesema haya.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Lakini siku moja, kama vile kile kigingi kilichofungwa mahali salama kitalegea kwa uzito, Eliakimu naye atapoteza madaraka yake na jamaa zake wote watabaki bila msaada. Mimi Mwenyezi-Mungu nimenena.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Lakini siku moja, kama vile kile kigingi kilichofungwa mahali salama kitalegea kwa uzito, Eliakimu naye atapoteza madaraka yake na jamaa zake wote watabaki bila msaada. Mimi Mwenyezi-Mungu nimenena.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Lakini siku moja, kama vile kile kigingi kilichofungwa mahali salama kitalegea kwa uzito, Eliakimu naye atapoteza madaraka yake na jamaa zake wote watabaki bila msaada. Mimi Mwenyezi-Mungu nimenena.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni asema, “Katika siku ile, kigingi kilichopigiliwa mahali imara kitaachia njia. Kitakatwa, nacho kitaanguka na mzigo ulioning’inia juu yake utaanguka chini.” Mwenyezi Mungu amesema.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 bwana Mwenye Nguvu Zote asema, “Katika siku ile, kigingi kilichogongomewa mahali imara kitaachia njia. Kitakatwa, nacho kitaanguka na mzigo ulioning’inia juu yake utaanguka chini.” bwana amesema.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

25 Katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, ule msumari uliokazwa katika mahali palipo imara utalegea; nao utakatwa na kuanguka chini, na ule mzigo uliokuwa juu yake utakatiliwa mbali; maana BWANA amesema haya.

Tazama sura Nakili

Isaya 22:25
15 Marejeleo ya Msalaba  

Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.

Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai.

Nami nitamkaza kama msumari mahali palipo imara; naye atakuwa kiti cha utukufu kwa nyumba ya baba yake.

Nao wataangika juu yake utukufu wote wa nyumba ya baba yake; wazao wake na watoto wao, kila chombo kidogo tangu vyombo vya vikombe hata vyombo vya makopo vyote pia.

Nikiita ndege mkali kutoka mashariki, mtu wa shauri langu toka nchi iliyo mbali; naam, nimenena, nami nitatekeleza; nimekusudia, nami nitafanya.

Mimi, naam, mimi, nimenena; naam, nimemwita; nimemleta, naye ataifanikisha njia yake.

Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi; kwa sababu mimi nimeyanena haya, na kuyakusudia, wala sikujuta wala mimi sitarudi nyuma niyaache.

Hivyo ndivyo ghadhabu yangu itakavyotimia, nami nitatosheleza hasira yangu juu yao, nami nitafarijika; nao watajua ya kuwa mimi, BWANA, nimenena kwa wivu wangu, nitakapokuwa nimeitimiza ghadhabu yangu juu yao.

Nayo itakuwa tukano na aibu, na mafundisho na ajabu, kwa mataifa wakuzungukao, hapo nitakapotekeleza hukumu ndani yako, kwa hasira, na kwa ghadhabu, na kwa adhabu kali; mimi, BWANA, nimeyanena hayo;

Nami nitatuma njaa na wanyama wabaya juu yenu, nao watakunyang'anya watu wako; na tauni na damu zitapita ndani yako; nami nitauleta upanga juu yako; mimi BWANA, nimeyanena hayo.

Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha BWANA wa majeshi kimesema hivi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo