Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Isaya 16:8 - Swahili Revised Union Version

8 Maana mashamba ya Heshboni yamenyauka, na mzabibu wa Sibma; mabwana wa mataifa wameyavunja matawi yake mateule; yamefika hadi Yazeri, yalitangatanga hadi jangwani matawi yake yalitapakaa, yaliivuka bahari.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Mashamba ya Heshboni yamefifia. Kadhalika na zabibu za Sibma ambazo ziliwalevya wakuu wa mataifa zikafika Yazeri na kusambaa hata jangwani, chipukizi zake zikafika hata ngambo ya bahari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Mashamba ya Heshboni yamefifia. Kadhalika na zabibu za Sibma ambazo ziliwalevya wakuu wa mataifa zikafika Yazeri na kusambaa hata jangwani, chipukizi zake zikafika hata ngambo ya bahari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Mashamba ya Heshboni yamefifia. Kadhalika na zabibu za Sibma ambazo ziliwalevya wakuu wa mataifa zikafika Yazeri na kusambaa hata jangwani, chipukizi zake zikafika hata ng'ambo ya bahari.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Mashamba ya Heshboni yananyauka, pia na mizabibu ya Sibma. Watawala wa mataifa wamekanyaga mizabibu iliyo mizuri sana, ambayo ilipata kufika Yazeri na kuenea kuelekea jangwani. Machipukizi yake yalienea yakafika hadi baharini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Mashamba ya Heshboni yananyauka, pia na mizabibu ya Sibma. Watawala wa mataifa wamekanyaga mizabibu iliyo mizuri sana, ambayo ilipata kufika Yazeri na kuenea kuelekea jangwani. Machipukizi yake yalienea yakafika hadi baharini.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Maana mashamba ya Heshboni yamenyauka, na mzabibu wa Sibma; mabwana wa mataifa wameyavunja matawi yake mateule; yamefika hadi Yazeri, yalitangatanga hadi jangwani matawi yake yalitapakaa, yaliivuka bahari.

Tazama sura Nakili

Isaya 16:8
13 Marejeleo ya Msalaba  

Enyi milima ya Gilboa, visiwepo juu yenu Umande wala mvua, wala mashamba ya matoleo; Maana ndipo ilipotupwa kwa aibu ngao ya shujaa, Ngao yake Sauli, pasipo kutiwa mafuta.

Lakini hivyo sivyo akusudiavyo mwenyewe, wala sivyo moyo wake uwazavyo; maana katika moyo wake akusudia kuharibu, na kukatilia mbali mataifa, wala si mataifa machache.

Heshboni analia na Eleale; mpaka Yahasa sauti ya kulia kwao inasikiwa; hata watu wa Moabu waliovaa silaha wanapiga kelele sana kwa sababu hiyo; nafsi yake inatetemeka ndani yake.

Basi, naililia mizabibu ya Sibma kwa kilio cha Yazeri, nitawanyeshea machozi yangu, Ee Heshboni na Eleale, kwa kuwa kelele za vita zimeyaangukia mavuno ya matunda yako, na mavuno ya mizabibu yako.

Divai mpya inaomboleza, mzabibu umedhoofika, watu wote waliochangamka moyo wanaugua.

Nitakulilia, Ee mzabibu wa Sibma, kwa vilio vipitavyo vilio vya Yazeri; matawi yako yalipita juu ya bahari, yalifika hadi bahari ya Yazeri; atekaye nyara ameyaangukia matunda yako ya wakati wa jua, na mavuno yako ya zabibu.

Kisha Musa akatuma watu ili kupeleleza Yazeri, nao wakaitwaa miji yake, wakawafukuza Waamori waliokuwamo.

Atarothi, na Diboni, na Yazeri, na Nimra, na Heshboni, na Eleale, na Sebamu, na Nebo na Beoni,

na Atrothi-shofani, na Yazeri, na Yogbeha;

na Nebo, na Baal-meoni, (majina yake yalikuwa yamegeuzwa) na Sibma; nao wakaiita miji waliyoijenga majina mengine.

na Kiriathaimu, na Sibma, na Sereth-shahari katika kilima cha hilo bonde;

Mpaka wao ulikuwa ni Yazeri, na miji hiyo ya Gileadi, na nusu ya nchi ya wana wa Amoni, mpaka Aroeri uliokabili Raba;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo