Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 13:22 - Swahili Revised Union Version

22 Na mbwamwitu watalia ndani ya ngome zake; na mbweha ndani ya majumba ya anasa; na wakati wake u karibu kufika, na siku zake hazitaongezeka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Mbwamwitu watalia ndani ya ngome zake, mbweha wataonekana ndani ya nyumba zao za anasa. Wakati wa Babuloni umekaribia, wala siku zake hazitaongezwa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Mbwamwitu watalia ndani ya ngome zake, mbweha wataonekana ndani ya nyumba zao za anasa. Wakati wa Babuloni umekaribia, wala siku zake hazitaongezwa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Mbwamwitu watalia ndani ya ngome zake, mbweha wataonekana ndani ya nyumba zao za anasa. Wakati wa Babuloni umekaribia, wala siku zake hazitaongezwa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Fisi watalia ndani ya ngome zake, mbweha ndani ya majumba yake ya kifahari. Wakati wake umewadia, na siku zake hazitaongezwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Fisi watalia ndani ya ngome zake, mbweha ndani ya majumba yake ya kifahari. Wakati wake umewadia, na siku zake hazitaongezwa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

22 Na mbwamwitu watalia ndani ya ngome zake; na mbweha ndani ya majumba ya anasa; na wakati wake u karibu kufika, na siku zake hazitaongezeka.

Tazama sura Nakili




Isaya 13:22
19 Marejeleo ya Msalaba  

Japo ulituponda katika pango la mbwamwitu, Na kutufunika kwa uvuli wa mauti.


Tena nitaifanya hiyo nchi kuwa makao ya nungunungu, na maziwa ya maji; nami nitaifagilia mbali kwa ufagio wa uharibifu; asema BWANA wa majeshi.


Kwa sababu umefanya mji kuwa ni rundo; Mji wenye boma kuwa ni magofu; Jumba la wageni kuwa si mji; Hautajengwa tena milele.


maana jumba la mfalme litaachwa; mji uliokuwa na watu wengi utakuwa hauna mtu; kilima na mnara utakuwa makao ya wanyama milele, furaha ya punda mwitu, malisho ya makundi ya kondoo;


Miiba itamea majumbani mwake, upupu na mbigili ndani ya maboma yake; nayo itakuwa kao la mbweha, na ua la mbuni.


Na hayawani wa nyikani watakutana na mbwamwitu, na beberu anamwita mwenziwe; naam, babewatoto anakaa huko na kupata pahali pa kustarehe.


Na mchanga ung'aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji; katika makao ya mbweha, walipokuwa wamelala, patakuwa na majani, pamoja na mianzi na manyasi.


Wanyama pori wataniheshimu, mbweha pia na mbuni; kwa sababu nimewapa maji jangwani, na mito nyikani, ili kuwanywesha watu wangu, wateule wangu;


Msiba wa Moabu umefika karibu, Na mateso yake wanamjia haraka.


Kwa maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi; Binti Babeli amekuwa kama sakafu ya kufikichia wakati wa kukanyagwa kwake; bado kitambo kidogo na wakati wa mavuno utafika kwake.


Nami nitafanya Yerusalemu kuwa magofu, Makao ya mbweha; Nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, Isikaliwe na mtu awaye yote.


Hata mbwamwitu hutoa matiti, Huwanyonyesha watoto wao; Binti ya watu wangu amekuwa mkali, Mfano wa mbuni jangwani.


Kwa ajili ya hayo nitaomboleza na kulia, Nitakwenda nimevua nguo, nikiwa uchi; Nitaomboleza kama mbweha, Na kulia kama mbuni.


Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.


Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; bundi na kunguru watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi.


Kisasi ni changu mimi, na kulipa, Wakati itakapoteleza miguu yao; Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka.


Na kwa tamaa yao watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; wao ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala maangamizi yao hayasinzii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo