Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 11:3 - Swahili Revised Union Version

3 na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Atafurahia kumcha Mwenyezi-Mungu. Hatahukumu kadiri ya mambo ya njenje, wala kuamua kufuatana na yale anayosikia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Atafurahia kumcha Mwenyezi-Mungu. Hatahukumu kadiri ya mambo ya njenje, wala kuamua kufuatana na yale anayosikia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Atafurahia kumcha Mwenyezi-Mungu. Hatahukumu kadiri ya mambo ya njenje, wala kuamua kufuatana na yale anayosikia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 naye atafurahia kumcha Mwenyezi Mungu. Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa macho yake, wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa masikio yake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 naye atafurahia kumcha bwana. Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa macho yake, wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa masikio yake,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;

Tazama sura Nakili




Isaya 11:3
20 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo mimi mjakazi wako nikasema, Neno la bwana wangu mfalme na liwe la kustarehesha; kwa kuwa kama malaika wa Mungu ndivyo alivyo bwana wangu mfalme, kuyapambanua yaliyo mema na yaliyo mabaya; naye BWANA, Mungu wako na awe pamoja nawe.


Mfalme akamwambia huyo mwanamke, Nenda nyumbani kwako, nami nitakufanyia agizo.


Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.


Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu watu hawa wako walio wengi?


Je! Sikio silo lijaribulo maneno, Kama vile kaakaa lionjavyo chakula?


Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno, Kama vile kaakaa lionjavyo chakula.


Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua Mungu.


Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, Na adili, na kila njia njema.


Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha BWANA ni hazina yake ya akiba.


Katika nchi hiyo itakuwa milki kwake katika Israeli; wala wakuu wangu hawatawaonea watu wangu tena kabisa; bali watawapa nyumba ya Israeli nchi hiyo, kwa kadiri ya makabila yao.


Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.


Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.


na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu.


Basi msihukumu kwa kuangalia kwa nje tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.


Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoeshwa kupambanua mema na mabaya.


Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo