Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 10:30 - Swahili Revised Union Version

30 Piga kelele sana, Ee binti Galimu; sikiliza, Ee Laisha; ole wako, maskini Anathothi!

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Pazeni sauti enyi watu wa Galimu! Tegeni sikio enyi watu wa Laisha! Jibuni enyi wenyeji wa Anathothi!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Pazeni sauti enyi watu wa Galimu! Tegeni sikio enyi watu wa Laisha! Jibuni enyi wenyeji wa Anathothi!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Pazeni sauti enyi watu wa Galimu! Tegeni sikio enyi watu wa Laisha! Jibuni enyi wenyeji wa Anathothi!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Piga kelele, ee Binti Galimu! Sikiliza, ee Laisha! Maskini Anathothi!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Piga kelele, ee Binti Galimu! Sikiliza, ee Laisha! Maskini Anathothi!

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

30 Piga kelele sana, Ee binti Galimu; sikiliza, Ee Laisha; ole wako, maskini Anathothi!

Tazama sura Nakili




Isaya 10:30
9 Marejeleo ya Msalaba  

Tena, mfalme akamwambia Abiathari kuhani, Nenda Anathothi mashambani kwako; kwa kuwa wastahili kufa; ila leo sikuui, kwa sababu wewe ulichukua sanduku la Bwana mbele ya Daudi baba yangu, na kwa sababu wewe uliteswa kwa mateso yote ya baba yangu.


Anathothi, Nobu, Anania;


Madmena ni mkimbizi; wenyeji wa Gebimu wamejikusanya wakimbie;


Maneno ya Yeremia, mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani waliokuwa katika Anathothi, katika nchi ya Benyamini;


Basi Hanameli, mwana wa mjomba wangu, akanijia ndani ya ukumbi wa walinzi, sawasawa na lile neno la BWANA, akaniambia, Tafadhali, ulinunue shamba langu lililoko Anathothi, katika nchi ya Benyamini; maana haki ya urithi ni yako, na haki ya ukombozi ni yako; ujinunulie. Ndipo nikajua kama neno hili ni neno la BWANA.


na Anathothi pamoja na mbuga zake za malisho, na Almoni pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne.


Wakauita mji jina lake Dani, kwa kulifuata jina la baba yao Dani, aliyezaliwa na Israeli; lakini jina la mji huo hapo awali lilikuwa Laisha.


Ndipo hao watu watano wakaenda zao, wakafika Laisha, wakawaona wale watu waliokuwamo ndani yake, jinsi walivyokaa kwa amani, kama ilivyokuwa desturi ya Wasidoni, watu watulivu na wasioshuku, wasiopungukiwa na chochote duniani, na waliokuwa na miliki; Nao walikuwa mbali na hao Wasidoni, wala hawakutangamana na watu wengine.


Lakini Sauli alikuwa amemposa Mikali, binti yake aliyekuwa mkewe Daudi, kwa Palti, mwana wa Laisha aliyekuwa mtu wa Galimu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo