Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Isaya 10:14 - Swahili Revised Union Version

14 Na mkono wangu umezitoa mali za mataifa kama katika kiota cha ndege; na kama vile watu wakusanyavyo mayai yaliyoachwa, ndivyo nilivyokusanya dunia yote; wala hapana aliyetikisa bawa, wala kufumbua kinywa, wala kulia.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Kama mtu anyoshaye mkono kwenye kiota, ndivyo nilivyochukua mali yao; kama mtu aokotavyo mayai yaliyoachwa kiotani, ndivyo nilivyowaokota duniani kote, wala hakuna mtu aliyeweza kupiga bawa, au aliyefungua kinywa kunipigia kelele.” Lakini Mwenyezi-Mungu asema hivi:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Kama mtu anyoshaye mkono kwenye kiota, ndivyo nilivyochukua mali yao; kama mtu aokotavyo mayai yaliyoachwa kiotani, ndivyo nilivyowaokota duniani kote, wala hakuna mtu aliyeweza kupiga bawa, au aliyefungua kinywa kunipigia kelele.” Lakini Mwenyezi-Mungu asema hivi:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kama mtu atiavyo mkono kwenye kiota, ndivyo mkono wangu ulivyochukua utajiri wa mataifa; kama watu wakusanyavyo mayai yaliyoachwa, ndivyo nilivyokusanya nchi zote; wala hakuna hata mmoja aliyepiga bawa au kufungua kinywa chake kutoa mlio.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

BIBLIA KISWAHILI

14 Na mkono wangu umezitoa mali za mataifa kama katika kiota cha ndege; na kama vile watu wakusanyavyo mayai yaliyoachwa, ndivyo nilivyokusanya dunia yote; wala hapana aliyetikisa bawa, wala kufumbua kinywa, wala kulia.

Tazama sura Nakili

Isaya 10:14
14 Marejeleo ya Msalaba  

Je! Ninyi hamjui mimi na baba zangu tuliyowafanyia watu wote wa nchi? Je! Miungu ya mataifa wa nchi iliweza kuokoa kwa lolote nchi zao na mkono wangu?

Kama nilifurahi kwa kuwa mali yangu ilikuwa nyingi, Na kwa sababu mkono wangu umepata vitu vingi;

Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

Yeye aliyewapiga mataifa kwa ghadhabu, Kwa mapigo yasiyokoma; Aliyewatawala mataifa kwa hasira, Ameadhibiwa asizuie mtu.

Nimechimba na kunywa maji, na kwa nyayo za miguu yangu nitaikausha mito yote ya Misri.

Ole wao waongezao nyumba baada ya nyumba, na kuweka shamba karibu na shamba, hadi ikawa hapana nafasi tena, nanyi ikawa hamna budi kukaa peke yenu katikati ya nchi!

Kuhusu kuogofya kwako, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Ushikaye kilele cha milima; Ujapofanya kiota chako juu sana kama tai, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.

Nanyi mmejitukuza juu yangu kwa vinywa vyenu, na kuyaongeza maneno juu yangu; nimesikia mimi.

Ujapopanda juu kama tai, Ijapokuwa kiota chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.

Chukueni nyara za fedha; Chukueni nyara za dhahabu; Kwa maana ni akiba isiyoisha, Fahari ya vyombo vipendezavyo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo