Hosea 2:7 - Swahili Revised Union Version7 Naye atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; atawatafuta, lakini hatawaona; ndipo atakaposema, Nitakwenda nikamrudie mume wangu wa kwanza; kwa maana hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema7 Atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; naam, atawatafuta, lakini hatawaona. Hapo ndipo atakaposema, “Nitarudi kwa mume wangu wa kwanza; maana hapo kwanza nilikuwa nafuu kuliko sasa.” Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND7 Atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; naam, atawatafuta, lakini hatawaona. Hapo ndipo atakaposema, “Nitarudi kwa mume wangu wa kwanza; maana hapo kwanza nilikuwa nafuu kuliko sasa.” Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza7 Atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; naam, atawatafuta, lakini hatawaona. Hapo ndipo atakaposema, “Nitarudi kwa mume wangu wa kwanza; maana hapo kwanza nilikuwa nafuu kuliko sasa.” Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu7 Gomeri atawafuatia wapenzi wake lakini hatawapata; atawatafuta lakini hatawapata. Kisha atasema, ‘Nitarudi kwa mume wangu kama kwanza, kwa maana nilikuwa na hali njema kuliko sasa.’ Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu7 Gomeri atawafuatia wapenzi wake lakini hatawapata; atawatafuta lakini hatawapata. Kisha atasema, ‘Nitarudi kwa mume wangu kama kwanza, kwa maana nilikuwa na hali njema zaidi kuliko sasa.’ Tazama suraBIBLIA KISWAHILI7 Naye atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; atawatafuta, lakini hatawaona; ndipo atakaposema, Nitakwenda nikamrudie mume wangu wa kwanza; kwa maana hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa. Tazama sura |
Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya.
ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa mwituni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng'ombe, nawe utanyeshewa na umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye Juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote.
Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda mwitu; akalishwa majani kama ng'ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye Juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote.